SIASA

SIASA

MAONI

MAONI

BURUDANI

MICHEZO

/ / KLOPP AONJA BAO LAKE LA KWANZA NA LIVERPOOL, LAKINI SARE!



LIGI KUU ENGLAND
MATOKEO:
Jumapili Oktoba 25
Sunderland 3 Newcastle 0              
Bournemouth 1 Tottenham 5       
Man United 0 Man City 0                 
Liverpool 1 Southampton 1                
++++++++++++++++++++++++++++             
LIVER-SOUTH-OKT25Jurgen Kloop, akiiongoza Liverpool kwa mara ya kwanza Uwanjani kwao Anfield tangu ateuliweMeneja, alishuhudia Timu yake ikipata Bao la kwanza chini yake lakini ikatoka Sare 1-1 na Southampton kwenye Mechi ya Ligi Kuu England.

Hadi Mapumziko, Gemu ilikuwa 0-0.
Liverpool walipata Bao lao Dakika ya 77 baada ya Krosi ya upande wa kulia iliyopigwa na James Milner kuunganishwa kwa Kichwa na Christian Benteke.

Southampton walisawazisha katika Dakika ya 86 baada ya Frikiki kumkuta Ramirez aliepiga kichwa Golini na Sadio Mane kuunganisha kwa kichwa hadi wavuni.

Kwenye Dakika za Majeruhi, Sadio Mane alitolewa nje kwa Kadi Nyekunda baada ya Kadi za Njano mbili.
Hadi mwisho, Liverpool 1 Southampton 1.
Hii ni Sare ya 8 katika Gemu 9 zilizopita za Liverpool katika Mashindano yote Msimu huu.

Matokeo haya yamewaweka Liverpool wakiwa Nafasi ya 7 wakiwa na Pointi 10 na Southampton wapo Nafasi ya 10 wakiwa na Pointi 13 huku zote zikicheza Mechi 10 kila mmoja.

VIKOSI:
Liverpool: Mignolet; Clyne, Skrtel, Sakho, Moreno; Lucas, Can; Milner, Coutinho, Lallana; Origi
Akiba: Toure, Benteke, Firmino, Allen, Ibe, Bogdan, Randall.

Southampton: Stekelenburg; Cedric Soares, Fonte, Van Dijk, Bertrand; Steven Davis, Clasie, Wanyama; Mane, Pelle, Tadic
Akiba: Kelvin Davis, Yoshida, Romeu, Ward-Prowse, Juanmi, Ramirez, Caulker.

REFA: Andre Marriner
LIGI KUU ENGLAND
RATIBA:
**Saa za Bongo
Jumamosi Oktoba 31
1545 Chelsea v Liverpool      
1800 Crystal Palace v Man United            
1800 Man City v Norwich                
1800 Newcastle v Stoke                  
1800 Swansea v Arsenal                 
1800 Watford v West Ham              
1800 West Brom v Leicester           
Jumapili Novemba 1
1630 Everton v Sunderland             
1900 Southampton v Bournemouth          
Jumatatu Novemba 2
2300 Tottenham v Aston Villa         

«
Next

Chapisho Jipya

»
Previous

Taarifa za zamani

About Unknown

Asante kwa kutembelea SELASINI HABARI,NITAKUHABARISHA, KUKUELIMISHA NA KUKUBURUDISHA HIVYO USIKOSE KUTEMBELEA SELASINIHABARI.BLOGSPOT.COM.

Hakuna maoni :

Leave a Reply