SIASA

SIASA

MAONI

MAONI

BURUDANI

MICHEZO

/ / Lulu Michael Alia Kwa Uchungu Akisimulia Jinsi Mama Yake Alivyompigania Akiwa Jela


Muigizaji wa filamu, Elizabeth Michael aka Lulu amelia kwa uchungu baada ya kukumbuka jinsi mama yake alivyompigania wakati yupo jela alikopelekwa kwa kusababisha kifo cha marehemu Steven Kanumba.

Akizungumza Ijumaa hii kwenye kipindi cha Uhondo cha EFM, Lulu alisema mama yake alifanya kila njia ili kuhakikisha mtoto wake anakuwa salama.

Mama yangu ana mapenzi pili ni jasiri,” alisema. “Ni mtu ambaye anaweza kusimama kwa kitu anachotaka kufanya na akafanikiwa. Sio mzazi mwenye mapenzi ya kumharibu mtoto. Hajali wewe ni Lulu wewe ni nani, Lulu mwisho getini, ukiingia ndani wewe ni mtoto,” aliongeza.

Tumepitia maisha fulani ambayo sio marahisi sana, kwahiyo nyakati tunazo nyingi lakini wakati ambao ulikuwa mgumu sana na akasimama wakati dunia nzima ilikuwa against, ni kitu ambacho kinanifanya niwe proud of her. Kipindi cha kesi yangu ni kipindi ambacho alitukanwa aliongelewa vibaya, ushirikina lakini alikubali akasema vyovyote vile lakini huyu ni mwanangu na akapigana na mpaka leo maisha yanaendelea,” alikumbushia Lulu huku akilia kwa uchungu.

«
Next

Chapisho Jipya

»
Previous

Taarifa za zamani

About Unknown

Asante kwa kutembelea SELASINI HABARI,NITAKUHABARISHA, KUKUELIMISHA NA KUKUBURUDISHA HIVYO USIKOSE KUTEMBELEA SELASINIHABARI.BLOGSPOT.COM.

Hakuna maoni :

Leave a Reply