SIASA

SIASA

MAONI

MAONI

BURUDANI

MICHEZO

/ / MALEJENDARI MAN UNITED WATOA HOTELI YAO KUSAIDIA WASIO NA MAKAZI.




NEVILLE-GIGGSWatu wapatao 30 ambao hawana makazi waliopiga kambi katika Jumba tupu linalomilikiwa na Mastaa Wawili wa zamani wa Manchester United wameruhusiwa kuendelea kukaa ndani yake hadi Majira ya Baridi yatakapomalizika.


NEVILLE-GIGGS-HOTEL
Gary Neville na Ryan Giggs wapo mbioni kulikarabati Jengo hilo la zamani la Soko la Hisa la Jijini Manchester ili kuligeuza kuwa Hoteli ya Kifahari.

Mwanaharakati wa Kutetea Haki za Binadamu, Wesley Hall, amesema aliongea kwa Simu na Gary Neville na akaambiwa Watu hao wasio na makazi wako huru kubaki Mjengoni humo bure hadi Februari wakati ukarabati wake utakapoanza.

Kundi hilo la Watu hao wasio na makazi walitimuliwa Mjengoni humo Wiki iliyopita lakini Hall alipofika hapo Majuzi Ijumaa alimkuta Mjenzi mmoja yuko hapo na Fundi huyo akampa Simu aongee moja kwa moja na Gary Neville.

Hall ameeleza: “Neville aliniambia hana tatizo Watu hao kukaa ndani ya Jumba hilo mradi walitunze!”
Hall amesema hisani hiyo ya Neville na Giggs ni kuwaokoa Watu hao masikini kuelekea kwenye kipindi kigumu cha baridi kali.

Mmoja wa Watu hao wasio na makazi waishio kwenye Jumba hilo, Wesley Dove, ambae amekuwa hana Nyumba kwa Miezi 12 na alikuwa akiishi kwenye Hema amesema kwa furaha na shukrani kubwa kuwa sasa wanaishi ndani ya Nyumba na watafanya kazi na kustirika na Majira ya Baridi.

Gary Neville, ambae sasa ni mmoja wa Makocha wa England na pia Mchambuzi wa Soka wa Kituoa cha TV cha Sky Sports, na Ryan Giggs, ambae ni Meneja Msaidizi wa Man United, wanataka kuligeuza Jumba hilo liwe Hoteli ya Kifahari ya Vyumba 35.

«
Next

Chapisho Jipya

»
Previous

Taarifa za zamani

About Unknown

Asante kwa kutembelea SELASINI HABARI,NITAKUHABARISHA, KUKUELIMISHA NA KUKUBURUDISHA HIVYO USIKOSE KUTEMBELEA SELASINIHABARI.BLOGSPOT.COM.

Hakuna maoni :

Leave a Reply