Bao
la Paul Aguilar katika Dakika ya 118 ndani ya Dakika za Nyongeza 30
limewapa Mexico ushindi wa Bao 3-2 na kutinga kwenye Mashindano ya FIFA
ya Kombe la Mabara yatakayochezwa huko Russia Mwaka 2017.
Kwenye Mechi hiyo iliyochezwa Alfajiri ya Leo huko Rose Bowl,
Pasadena, USA, mbele ya Watu 93,723, Mexico walianza kufunga kwa Bao la
Dakika ya 10 la Javier Hernandez 'Chicharito' na USA kusawazisha Dakika
ya 15 kupitia Geoff Cameron.
Bao hizo zilidumu hadi Dakika 90 kwisha na ndipo Dakika za Nyongeza
30 zikachezwa na Mexico kuibwaga USA kwa mara ya kwanza katika Mechi 7
walizokutana chini ya Kocha wa USA Jurgen Klinsmann.
===============
MAGOLI:
USA 2
-Geoff Cameron Dakika ya 15
-Bobby Wood 108
MEXICO 3
-Chicharito Dakika ya 10
-Oribe Peralta 96
-Paul Aguikar 118
===============
Mechi hii ilizikutanisha Washindi waliopita wa Mashindano ya
CONCAFA CUP ili kupata Timu moja kuwakilisha Bara hili la FIFA la Nchi
za Marekani ya Kati na Kaskazini na Nchi za Visiwa vya Carribean ili
kucheza Mashindano ya FIFA ya Kombe la Mabara huko Russia Mwaka 2017.
Kombe la Mabara huchezwa Mwaka mmoja kabla ya Fainali za Kombe la
Dunia na kwa vile Fainali zijazo zitachezwa Russia Mwaka 2018 Kombe hili
litachezwa huko huko Russia kuanzia Tarehe 17 Juni 2017 hadi Julai 2,
2017.
Washiriki wa Kombe la Mabara 2017 ni Wenyeji Russia, Mabingwa wa
Dunia Germany, Mexico na Wawakilishi wengine Watano toka Mabara mengine
ya FIFA kama vile CAF, AFC, OFC, CONMEBOL na UEFA.
Hakuna maoni :