SIASA

SIASA

MAONI

MAONI

BURUDANI

MICHEZO

/ / SIKILIZA ANACHOKISEMA KIIZA KUHUSIANA NA KAVUMBAGU KUJIUNGA SIMBA...


Mshambulizi wa Simba, Mganda, Hamis Kiiza, amemkaribisha Mrundi wa Azam FC, Didier Kavumbagu, kujiunga na timu hiyo inayofundishwa na Muingereza, Dylan Kerr.

Hiyo ni siku chache tangu ziwepo tetesi za Mrundi huyo kuomba kujiunga na Simba kwenye usajili wa dirisha dogo msimu huu kwa mkopo.

Mrundi huyo, hivi sasa hana nafasi ya kucheza kwenye kikosi cha kwanza tangu kuanza kwa msimu huu wa Ligi Kuu Bara, kwa kile kinachodaiwa kuwa mshambuliaji huyo ameshindwa kumudu mfumo wa Kocha Mkuu Muingereza, Stewart Hall.


Kiiza alisema kuwa, anatambua uwezo wa mshambuliaji huyo ndani ya uwanja, hivyo anaamini akitua kuichezea timu hiyo, ataiboresha safu yao ya ushambuliaji.
Kiiza alisema kikubwa anataka kuona safu yao ya ushambuliaji inaimarika kwa kuwepo na washambuliaji wenye uwezo mkubwa wa kufunga mabao.

 “Katika timu lazima wawepo washambuliaji zaidi ya watatu ambao ni tishio kwa wapinzani, lakini siyo kuwepo mmoja ambaye mabeki wa timu pinzani wenyewe wanamuangalia yeye tu katika kumkaba.

“Hivyo kama Kavumbagu anataka kuja Simba, mimi namkaribisha, ni mshambuliaji mzuri niliyecheza naye timu moja ya Yanga, ana uwezo mkubwa wa kufunga mabao, pia anajua kupambana,” alisema Kiiza.

«
Next

Chapisho Jipya

»
Previous

Taarifa za zamani

About Unknown

Asante kwa kutembelea SELASINI HABARI,NITAKUHABARISHA, KUKUELIMISHA NA KUKUBURUDISHA HIVYO USIKOSE KUTEMBELEA SELASINIHABARI.BLOGSPOT.COM.

Hakuna maoni :

Leave a Reply