SIASA

SIASA

MAONI

MAONI

BURUDANI

MICHEZO

/ / TAIFA STARS KAMA KAWA, KAMA DAWA, YASONGA SASA NI ALGERIA NOVEMBA



Taifa Stars imepoteza mechi yake dhidi ya Malawi kwa kufungwa bao 1-0 mjini Blantyre, lakini imesonga mbele katika mechi hizo za awali kuwania kucheza Kombe la Dunia mwaka 2018 nchini Urusi.
Stars imesonga mbele kwa jumla ya mabao 2-1 baada ya ushindi wake wa mabao 2-0 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam
 Jijini Dar es Salaam, Jumatano.

Malawi ilipata bao lake mwishoni mwa kipindi cha kwanza kupitia shuti kali la John Banda lililombabatiza Kelvin Yondani na kumshinda kipa Ally Mustapha.

Hata hivyo kipa huyo aliendelea kuwa shujaa kwa kuokoa michomo mingi katika kipindi cha kwanza ambacho Malawi walikuwa vizuri zaidi.
Stars walitumia muda mwingi kukaba hasa katika kipindi cha kwanza, angalau katika kipindi cha pili wakaanza kuonyesha mabadiliko kwa kupambana zaidi.

Kutokana na ushindi huo, Stars inatarajia kucheza mechi mbili dhidi ya Algeria ambazo zitachezwa kati ya Novemba 9 na 17.

«
Next

Chapisho Jipya

»
Previous

Taarifa za zamani

About Unknown

Asante kwa kutembelea SELASINI HABARI,NITAKUHABARISHA, KUKUELIMISHA NA KUKUBURUDISHA HIVYO USIKOSE KUTEMBELEA SELASINIHABARI.BLOGSPOT.COM.

Hakuna maoni :

Leave a Reply