SIASA

SIASA

MAONI

MAONI

BURUDANI

MICHEZO

/ / Uchumba wa Wastara Wavunjika...Wastara Achoka na Usaliti wa Bond



Uchumba wa mastaa wa filamu za Kibongo, Wastara Juma na Bond Bin Suleiman ambao ulikuwa umepamba moto huku hivi karibuni ikidaiwa wataoana baada ya uchaguzi, umevunjika baada ya Wastara kusalitiwa.

Chanzo makini kilichoomba hifadhi ya jina lake kilidai kuwa, wawili hao walikuwa wakienda vizuri lakini hivi karibuni Bond alibainika kumsaliti mwezake kwa kuwa na mwanamke mwingine aliyezaa naye.

Uchumba wao ulikuwa unaenda vizuri tu lakini mara kwa mara Bond amekuwa akimliza mwenzake kwa kuchepuka. Wastara akawa anaziba masikio kwa kuwa anampenda.

“Kuna wakati Bond alidaiwa kumpa mimba mwanamke aliyefahamika kwa jina la Grace, Wastara akafunika, sasa naona amechoka maana inadaiwa Bond ana mtoto mdogo aliyezaa na mwanamke mwingine.

Baada ya habari hizi kutua kwenye dawati la gazeti hili, mwandishi wetu alimwendea hewani Wastara ambaye alikiri kusikia habari za Bond kuwa na mtoto ila akasema anafuatilia na akijua ukweli atalazimika kujiweka pembeni.

Mh! Kama hizo habari na nyinyi zimewafikia basi, maana mimi nilizisikia kijuu juu nikaona nitazifanyia kazi ila kiukweli kama ni hivyo, najiweka pembeni. Nimekuwa nikimpigia simu lakini simpati kwa takriban wiki nzima sasa, sijui shida iko wapi,” alisema Wastara.

Source:Global Publishers

«
Next

Chapisho Jipya

»
Previous

Taarifa za zamani

About Unknown

Asante kwa kutembelea SELASINI HABARI,NITAKUHABARISHA, KUKUELIMISHA NA KUKUBURUDISHA HIVYO USIKOSE KUTEMBELEA SELASINIHABARI.BLOGSPOT.COM.

Hakuna maoni :

Leave a Reply