Waziri wa Maji na Umwagiliaji,Profesa Jumanne Maghembe akizungumza wakati wa kuzindua Bodi ya Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Saalam(Dawasa)jijini Arusha,katikati ni Mwenyekiti wa Bodi ya Majisafi na Usafi wa Mazingirajiji la Arusha(Auwsa)Felix Mrema na Katibu Mkuu wizara ya Maji,Mhandisi Mbogo Mfutakamba. |
Katibu Mkuu wizara ya Maji,Mhandisi Mbogo Mfutakamba akizungumza wakati wa kuzindua Bodi ya Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Saalam(Dawasa) jijini Arusha. |
Afisa Mtendaji Mkuu wa Dawasco,Mhandisi Cyprian Luhemeja(kushoto)akijadilia jambo na Mwenyekiti wa Bodi ya Majisafi na Usafi wa Mazingirajiji la Arusha(Auwsa)Felix Mrema(kulia) na Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa mazingira,Mhandisi Ruth Koya wakati wa uzinduzi wa Bodi ya Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Saalam(Dawasa) jijini Arusha |
WAZIRI wa Maji,Profesa Jumanne Maghembe amezindua Bodi mpya ya
Wakurugenzi
wa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam(Dawasa) na kuitaka
kuhakikisha wanafanyakazi kwa bidii katika mfumo wa Matokeo Makubwa Sasa
ili kuondoa kero ya maji kwa wananchi.
Maghembe
alitoa kauli hiyo jijini Arusha na kusema kuwa serikali imepata kiasi
cha dola za Marekani 409 kutoka Benki ya Dunia,Korea Kusini na wadau
wengine kuweka miundombinu ya majitaka itakayosaidia kupunguza uchafuzi
wa mazingira kwenye bahari ya Hindi.
Alisema
idadi ya watu katika jiji la Dar es Salaam inaongezeka kila mara hiyo
serikali imejipanga kuhakikisha inatengeneza miundombinu itakayowezesha
upatikanaji wa maji safi na maji taka unaondana na hadhi ya jiji.
“Benki
ya Dunia imetoa kiasi cha dola 220 milioni na Serikali ya Korea ya
Kusini dola 89 milioni ambazo zitasaidia kwa kiwango kikubwa kukabiliana
na changamoto ya mahitaji ya maji na uboreshaji miundombinu ya Maji
taka,”alisema Profesa Maghembe
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Maji,Mhandisi Mbogo Mfutakamba alisema kumekua na
maboresho makubwa baada ya kuchimbwa visima virefu kwenye maeneo ya
Kimbiji na Mpera hatua ambayo imewapa wananchi maji kwa kiwango cha kuridhisha kufikia asilimia 68 ya mahitaji.
Mwenyeketi wa Bodi ya Wakurugenzi (Dawasa)Dk, Eve Sinare alisema watashirikiana na Menejimenti kukabiliana na changamoto za maji kwa kushirikiana Dawasco na wadau wengine.
Alisema
katika kipindi kilichopita bodi yake ilipata mafanikio kutokana na
kutokuingilia Menejimenti katika utendaji kazi kwani sio jukumu la bodi
kuingilia utendaji wa Dawasa wa siku kwa siku.
Hakuna maoni :