Na Anitha Jonas –MAELEZO
SERIKALI imeandaa mkakati wa kuzuia Homa ya Bonde la Ufa (Rift Valley Fever) nchini kutokana na kuwepo na viashiria vya kuwepo na ungojwa huo katika kipindi hiki cha mvua za Eli-nino kama ilivyoripotiwa na Mamlaka ya hali ya hewa.
SERIKALI imeandaa mkakati wa kuzuia Homa ya Bonde la Ufa (Rift Valley Fever) nchini kutokana na kuwepo na viashiria vya kuwepo na ungojwa huo katika kipindi hiki cha mvua za Eli-nino kama ilivyoripotiwa na Mamlaka ya hali ya hewa.
Ugongwa
wa Homa ya Bonde la Ufa ni hatari sana na kwani katika kipindi cha
2006/2007 ulipotokea ulisambaa kwa kasi na kuathiri vijiji 175 kati ya
wilaya 11 katika ya Ukanda wa Kati na Ukanda wa Kaskazini Mashariki mwa
nchi.
Hayo
aliyasema hivi karibuni Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Maendeleo ya
Uvuvi Dkt.Yohana Budeba alipokuwa akifungua mkutano wa wataalamu kutoka
sekta mbalimbali wanaoandaa mkakati wa kupapamba na Homa ya Bonde la Ufa
nchini.
“Serikali
imeamua kuchukua tahadhari ya haraka ili kuepuka mlipuko wa ugongwa wa
Homa ya Bonde la Ufa,kutokana na kuwepo na taarifa za mvua za
Eli-nino,kamati inaandaa mkakati wa kuanza tuoa elimu kwa umma juu ya
ugonjwa huu pamoja kutoa chanjo kwa wanyama,pamoja na kuweka dawa katika
majoshi ya mifugo kama ngombe,mbuzi na kondoo halikadhalika kupulizia
dawa kwa mifugo katika maeneo ya minada”,alisema Dkt Budeba.
Kwa
upande wa Mkurugenzi wa Huduma za Mifugo kutoka katika Wizara ya
Mifugo na Maendeleo ya Uvuvi Dkt.Abdu Hayghaimo alisema Homa ya Bonde la
Ufa ni ungonjwa ambao huambukiza kutoka kwa mnyama na kwenda kwa
binadamu kwa kula nyama ya mfugo aliyeathirika na ugongwa ,pia
husababishwa na aina ya mbu ambao huuma nyakati za mchana .
“Ninaomba
kuwasihi watanzania wote kutoa taarifa katika kwa wataalamu wa Mifugo
sehemu yoyote wanapoona dalili kama mimba za mifugo kama ngombe,mbuzi na
kondoo kutoka kwani hiyo ni dalili moja wapo ya ugongwa wa Homa ya
Bonde la Ufa”, alisema Dkt. Hayghaimo.
Mbali
na hayo Dkt Budeba alitoa pongezi kwa Mamlaka ya Hali ya hewa kwa kazi
nzuri wanayoifanya ya kutoa taaarifa zenye kuonyesha ukweli
ikiwa tayari dalili za mvua za Eli-nino zimeanza kuonekana nchini
katika maeneo mbalimbali.


Hakuna maoni :