Mahakama ya hakimu mkazi Morogoro imemuachia huru Katibu wa Jumuiya na
Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Issa Ponda aliyekuwa akituhumiwa
kwa makosa ya uchochezi baada ya mahakama kutoridhishwa na ushahidi wa
upande wa mashtaka na hivyo kuonekana hana hatia
Makosa yaliyokuwa yakimkabili ni mawili ambayo ni kushawishi watu
kutenda kosa, pamoja na kutoa matamshi yanayoumiza imani ya dini
nyingine.
Hakimu wa kesi hiyo Mary Moyo amesema ushahidi uliotolewa na upande wa
mashitaka haukujitosheleza hivyo mahakama hiyo imemwachia huru na rufaa
iko wazi endapo upande wa mashitaka hautaridhika na hukumu hiyo.
Tagged with: MATUKIO
Hakuna maoni :