MENEJA
wa England Roy Hodgson ametangaza kwamba Wayne Rooney hataanza kwenye
Mechi ya Kirafiki na Spain ya Ijumaa huko Alicante Nchini Spain.Mbali ya kutamka hilo, Hodgson pia amedokeza kuwa Mfungaji Bora wa Ligi Kuu England, Jamie Vardy, pia yupo mashakani kucheza Mechi hiyo kutokana na maumivu.
Hata hivyo, Hodgson amesisitiza kutoanza Mechi hiyo kwa Rooney ni kwa sababu tu anataka kuwapa nafasi Wachezaji wengine kuonyesha uwezo wao kabla hajateua Kikosi chake cha kucheza Fainali za EURO 2016 Mwezi Juni huko France.
Hodgson ametoboa kuwa Rooney ataanza Mechi ya Kirafiki ya Jumanne dhidi ya France Uwanjani Wembley Jijini London.
Akiongea na Wanahabari, Hodgson amesema: “Wayne yupo na mimi hii Leo kwa sababu ndie Kepteni wangu. Ni Mtu muhimu lakini hataanza Mechi ya Kesho. Tunaangalia Wachezaji wengine lakini ataanza Mechi na France Jumanne.”
Nae Rooney amekiri umuhimu wa kubadili Wachezaji kwenye Kikosi ili Meneja apate kupima kila Mchezaji.
Kuhusu Jamie Vardy ambae amepiga Bao katika Mechi zake 9 zilizopita za Ligi Kuu England anasumbuliwa na maumivu baada ya kuumia kwenye Mechi ya Jumamosi iliyopita Timu yake Leicester City ilipoifunga Watford.
Wikiendi hii, mbali ya hii ya Spain na England, zipo Mechi za Kimataifa za Kirafiki huku kadhaa zikiwa Bigi Mechi kama vile France v Germany, Belgium v Italy, England v France, Belgium v Spain na Germany v Netherlands ambazo zitapigwa Ijumaa na Jumanne.
KIMATAIFA KIRAFIKI
Ratiba
*Saa za Bongo
Jumatano Novemba 11
15:00 Jordan v Malta
20:00 Estonia v Georgia
Alhamisi Novemba 12
17:00 Oman v New Zealand
19:00 Macedonia v Montenegro
20:00 Andorra v Saint Kitts And Nevis
Ijumaa Novemba 13
3:00 Solomon Islands v Fiji
20:30 Qatar v Turkey
21:00 Luxembourg v Greece
21:45 Poland v Iceland
21:45 Northern Ireland v Latvia
21:45 Belgium v Italy
21:45 Portugal v Russia
22:30 Czech Republic v Serbia
22:45 Spain v England
22:45 Slovakia v Switzerland
22:45 Wales v Netherlands
23:00 France v Germany
Jumamosi Novemba 14
10:00 Hong Kong v Macau
Jumanne Novemba 17
Tuesday 17 Nov 2015
3:00 Italy v Poland
3:00 Lebanon v New Zealand
14:00 Macedonia v Lebanon
18:00 Russia v Croatia
19:00 Estonia v Saint Kitts And Nevis
19:00 Azerbaijan v Moldova
20:15 Turkey v Greece
21:30 Luxembourg v Portugal
21:45 Austria v Switzerland
21:45 Poland v Czech Republic
21:45 Slovakia v Iceland
21:45 Belgium v Spain
22:00 England v France
22:45 Germany v Netherlands
22:45 Italy v Romania

Hakuna maoni :