Baada ya kuteuliwa na CCM na kupita katika mchakato wa kumpata mgombea
Uspika wa Bunge la Kumi na moja bila kupingwa, Job Ndugai ameeleza
changamoto anazotarajia kukutana nazo ikiwa ni pamoja na migomo.
Akiongea na waandishi wa habari jana baada ya jina lake kupitishwa,
Ndugai alilielezea Bunge la kumi na moja kama Bunge lenye utofauti
mkubwa na mabunge mengine huku akidai kuwa ongozeko la vijana wengi na
wasomi wengi zaidi kunaashiria kuongezeka kwa changamoto zaidi.
“Bunge hili lina wabunge wengi vijana, lina wabunge wengi wasomi zaidi
kuliko mabunge yote yaliyowahi kutokea na lina uwakilishi mkubwa. Hili
ni Bunge ambalo litakuwa na changamoto nyingi, tetegemee migomo ya hapa
na pale, hata hivyo ubora wa kazi utakuwa mkubwa,” alisema Ndugai.
Hata hivyo, Ndugai alisisisitiza kuwa ataliongoza Bunge kwa weledi na
kutenda haki kwa kila upande hivyo aliwataka wabunge wote wakiwemo wa
upinzani kumuunga mkono leo ili awe Spika wa Bunge la 11.
Home
/
SIASA
/
Job Ndugai Aanza Kuweweseka...Adai Tutegemee Migomo ya Hapa na Pale Katika Bunge Lijalo...Kisa Hichi Hapa
Job Ndugai Aanza Kuweweseka...Adai Tutegemee Migomo ya Hapa na Pale Katika Bunge Lijalo...Kisa Hichi Hapa
Tagged with: SIASA


Hakuna maoni :