SIASA

SIASA

MAONI

MAONI

BURUDANI

MICHEZO

/ / JOSE MOURINHO NA DIEGO COSTA WAPANDISHIANA KWENYE MECHI!

costa 0BOSI wa Chelsea Jose Mourinho amesema yeye na Diego Costa wameshapatana baada ya kukwaruzana wakati wa Mechi ya UEFA CHAMPIONZ LIGI, UCL, Jana Usiku walipoidunda Maccabi Tel Aviv 4-0 katika Mechi ya Kundi G.
 
Mourinho hakuridhishwa na kiwango cha Costa katika Kipindi cha Kwanza cha Mechi hiyo.
 
Meneja huyo alieleza: “Nilisikitishwa. Nikabwata na yeye akajibu. Lakini haftaimu tulikuwa kitu kimoja na kupongezana.”
 
Bao za Chelsea hiyo Jana zilifungwa na Gary Cahill, Willian, Oscar na Kurt Zouma.
 
Ushindi huu umeifanya Chelsea wafikishe Pointi 10 sawa na FC Porto ambao Jana walipigwa 2-0 na Dynamo Kiev.
 
Chelsea na FC Porto zitakutana kwenye Mechi ya mwisho ya Kundi G Uwanjani Stamford Bridge hapo Desemba 9 na Kikosi cha Mourinho kinahitaji Sare tu ili kutinga Raundi ya Mtoano ya Timu 16 ya UCL.
 
Wakati huo huo, Mourinho ametoboa kuwa Nahodha wao John Terry aliumia Enka kwenye Mechi hiyo na Maccabi na yupo hatarini kuikosa Mechi ya Ligi Kuu England Jumapili huko White Hart Lane dhidi ya Tottenham.

«
Next

Chapisho Jipya

»
Previous

Taarifa za zamani

About Unknown

Asante kwa kutembelea SELASINI HABARI,NITAKUHABARISHA, KUKUELIMISHA NA KUKUBURUDISHA HIVYO USIKOSE KUTEMBELEA SELASINIHABARI.BLOGSPOT.COM.

Hakuna maoni :

Leave a Reply