BEN SAANANE ambaye ni mkuu wa Idara ya sera na utafiti wa chadema
akionyesha baadhi ya picha za mauaji ya viongozi wa Chama hicho
yaliyowahi kufanyika na hakuna hatua zozote zilizochukuliwa hadi sasa
jambo ambalo sasa wamesema wamechoka na wameamua kujilinda wenyewe kwa
kuhakikisha kuwa wanawakamata wale wote walioendesha tukio la GEITA
**************
Baraza la vijana la chama cha Demokocrasia na maendeleo chadema BAVICHA
wametoa siku tatu kwa jeshi la polisi nchini kumwachia Mwenyekiti wa
baraza hilo PATROBAS KATAMBI aliyekamatwa jana mkaoni mwanza pamoja na
kuwakamata wahusika wote waliohusika na kifo cha Mwenyekiti cha CHADEMA
mkoani GEITA Bwana ALPHONCE MAWAZO huku wakisema kuwa kama hayo
hayatafanyika watalazimika kulipa kisasi.
Akizungumjza na wanahabari mchana wa leo jijini Dar es salaam katibu wa
uenezi wa baraza hilo Taifa Bwana EDWARD SIMBEYE amesema kuwa kwa sasa
vijana na wanachama wa chadema wamechoka na mauaji ya viongozi wa chama
hicho huku kukiwa hakuna hatua zinazochukuliwa kwa wahusika hivyo sasa
wameamua kuhakikisha kuwa wanajilinda wenyewe ikiwa ni pamoja na
kuwatafuta wahusika wa tukio la Geita na kuwakamata kama polisi watakuwa
wameshindwa kufanya hivyo kwa muda muafaka..
Akizungumzia tukio la jana mkoani mwanza amesema kuwa wakati jana mwili
wa marehemu MAWAZO ukiwasili katika hospitali ya BUGANDO kwa ajili ya
kuhifadhiwa na kufanyiwa uchunguzi zaidi Polisi walipanga njama za
kuutorosha mwili wa marehemu kwa ajili ya kwenda kuuzika kimya kimya
jambo ambalo amesema wanachama na viongozi wa CHADEMA walishtuka na
kuamua kulinda mwili huo na ndipo ilipotokea vurugu iliyopelekea
kiongozi wa vijana taifa kukamatwa na polisi .
Amesema kuwa inashangaza kuona jeshi la polisi likiwa katika mstari
wambele kuhangaika juu ya mwili wa Marehemu ALPHONCE MAWAZO wakati iko
wazi kuwa wakati anauawa na wananchi polisi walikuwepo eneo la tukio na
kushindwa kutoa hata msaada wa gari kwa ajili ya kumpeleka hospitalini
lakini jana polisi walipata gari la kuja kumtorosha katika hospitali
hiyo jambo ambalo amesema limekuwa likifanywa na polisi kila mara
yanapotokea matukio ya mauaji kama haya.
Aidha katika hatua nyingine vijana hao wametangaza rasmi kuwa baada ya
siku tatu na polisi kushindwa kuwaachia huru viongozi wao na kuwakamata
wauaji wa MAWAZO wamewaagiza vijana wote wa Tanzania kukusanyika kwa
wingi mkaoni mwanza kwa ajili ya kushinikiza kuwaachia viongozi wao
pamoja na kulinda mwili wa marehemu ALPHONCE MAWAZO ambao umelazwa
katika hospitali ya Bugando mkoani mwanza.
Marehemu ALPHONCE MAWAZO aliuawa na wananchi mkoani GEITA baada ya
kushambuliwa na wananchi waliokuwa na sialaha za jadi ambao hadi sasa
hakuna taarifa rasmi inayoeleza hali halisi ya mauaji hayo
Tagged with: SIASA

Hakuna maoni :