SIASA

SIASA

MAONI

MAONI

BURUDANI

MICHEZO

/ / CHALENJI CUP: KIBADENI ATANGAZA 21 WA KILIMANJARO STARS!


TFF-KIBADEN-MKWASAKocha mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania bara ‘Kilimanjaro Stars’, Abdallah Kibadeni ametangaza kikosi cha wachezaji 21 kujiandaa na michuano ya Kombe la Chalenji itakayoanza kutimua vumbi Jumamosi Novemba 21, nchini Ethiopia.

Kibadeni anayesaidiwa na kocha msaidizi Juma Mgunda, amesema wachezaji aliowaita wapo katika hali nzuri na wamekua wakifanya mazoezi na kikosi cha Taifa Stars ambapo wao kama benchi la ufundi wamepata nafasi ya kuwa nao kwa muda mrefu na kutambua maendeleo yao.

“Tumechagua wachezaji kulingana na mahitaji ya timu, tumekua na wachezaji hawa kwa muda mrefu katika vipindi mbalimbali, tuna amini tuliowachagua watafanya vizuri katika michuano hiyo mikongwe barani Afrika” amesema Kibadeni.

Wachezaji walioitwa ni magolikipa, Ally Mustafa (Yanga) na Aishi Manula (Azam), Said Mohamed (Mtibwa Sugar), walinzi Shomari Kapombe (Azam), Hassan Kessy (Simba), Mohamed Hussein (Simba), Hassan Isihaka (Simba), Salim Mbonde (Mtibwa), Juma Abdul (Yanga) na Kelvin Yondani (Yanga).
Viungo Himid Mao (Azam), Jonas Mkude (Simba), Said Ndemla (Simba), Salum Telela (Yanga), Salum Abubakar (Azam), Deus Kaseke (Yanga), washambuliaji John Bocco (Azam), Elias Maguri (Stand United), Ibrahim Hajibu (Simba), Malimi Busungu (Yanga) na Saimon Msuva (Yanga).

Michuano ya Kombe la Chalenji inatarajiwa kuanza kutimua vumbi Novemba 21 na kumalizika Disemba 6, ambapo Kilimanjaro Stars imepangwa kundi A, lenye wenyeji Ethiopia, Rwanda na Somalia.

Wachezaji Said Mohamed, Juma Abdul, Hassan Kessy, Hassan Isihaka, Salum Abubakar na Ibrahim wanaendelea na mazoezi jijini Dar es salaam chini ya kocha msaidizi Juma Mgunda wakati wanawasubiri wachezaji wengine walioko nchini Algeria na kikosi cha Taifa Stars.

Kundi B lina Bingwa Mtetezi Kenya, Burundi, Uganda na Zanzibar, huku kundi C likiundwa na timu za Sudan, Sudani Kusini, Djibouti na waalikwa wa michuano hiyo timu ya taifa kutoka Malawi.

SDL KUENDELEA NOVEMBA 28
Ligi Daraja la Pili nchini (SDL) imeanza kutimua vumbi jana katika viwanja 12 mikoa mbali, huku timu 24 zikisaka nafasi nafasi nne za kupanda Ligi Daraja la Kwanza msimu ujao wa 2016/2017.
Katika michezo iliyochezwa jana matokeo yalikuwa ni Alliance 2 -0 Madini, JKT Rwamkoma 1- 3 Bulyanhulu, Mvuvuma 0 – 0 Green Warriors, Singida United 1 -0 Transit Camp, Mirambo 1 – 0 Abajalo Tabora.
Karikaoo 1 – 0 Cosmopolitan, Mshikamano 1- 1 Changanyikeni, Villa Squad 0 – 2 Abajalo Dar es salaam, Mkamba Ranger 0 -0 The Mighty Elephant, Sabasaba 0 - 1 Mbeya Warriors, Wenda 0 – 0 African Wanderes.
Ligi hiyo inatarajiwa kuendelea Novemba 28, kwa timu 24 kucheza katika viwanja 12 mbalimbali nchini kusaka pointi muhimu.
IMETOLEWA NA TFF

«
Next

Chapisho Jipya

»
Previous

Taarifa za zamani

About Unknown

Asante kwa kutembelea SELASINI HABARI,NITAKUHABARISHA, KUKUELIMISHA NA KUKUBURUDISHA HIVYO USIKOSE KUTEMBELEA SELASINIHABARI.BLOGSPOT.COM.

Hakuna maoni :

Leave a Reply