RAIS
mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete
amesema hatashangaa rais wa sasa, Dk John Pombe Magufuli kwenda Uwanja
wa Taifa, Dar es Salaam Jumamosi kushuhudia mchezo dhidi ya Algeria.
Tanzania,
‘Taifa Stars’ itamenyana na Algeria, ‘Mbweha wa Jangwani’ Jumamosi
kabla ya kurudiana Novemba 17 mjini Algiers na mshindi wa jumla ataingia
kwenye makundi ya kuwania tiketi ya Kombe la Dunia 2018 Urusi.
Na
akizungumza nyumbani kwake, Msoga, Bagamoyo mkoani Pwani, Rais mstaafu
Kikwete amesema hatashangaa Rais wa sasa, Dk Magufuli akienda kushuhudia
mchezo huo, kwa sababu naye ni mpenzi wa michezo.
“Sitashangaa
hata rais wetu, Dk John Pombe Magufuli akienda kuongoza Watanzania
kuishangilia Taifa Stars, maana naye anapenda michezo,”alisema Kikwete
jana akizungumza na Ujumbe wa Kamati ya Taifa Stars uliomtembelea
nyumbani kwake.
| Rais Mstaafu Dk. Jakaya Mrisho Kikwete (kulia) akiwa Rais Dk. John Pombe Magufuli |
Akiuzungumzia
mchezo huo, Dk Kikwete amesema kwamba anaamini Taifa Stars inaweza
kuifunga Algeria japokuwa ndiyo bora kwa sasa Afrika, kikubwa ni uteuzi
wa wachezaji bora na maandalizi mazuri.
“Wahenga
wana msemo wao mmoja kwamba, Hata bahari kubwa huvukwa, basi nami
naamini tunaweza kuifunga Algeria, kikubwa watu wajitokeze kwa wingi
kuisapoti timu Jumamosi, kwa sababu shabiki ni mchezaji wa 12,”amesema
Rais Kikwete.
Dk
Kikwete aliyeondoka madarakani rasmi Novemba 5, mwaka huu baada ya
kuiongoza Tanzania kwa miaka 10, akimrithi Benjamin William Mkapa,
amesema katika kusaidia kampeni ya Taifa Stars dhidi ya Algeria naye
atatoa mchango wake.
“Nami
nitachangia, lakini si kwa kiwango kikubwa, kwa sababu mimi sasa hivi
ni mstaafu, naishi kwa pensheni. Nilipokuwa madarakani nilisaidia sana
na nilihamasisha watu kuipenda timu yao ya taifa, nilivaa hadi jezi za
timu ya taifa ili kuwashawishi watu kuipenda timu yao,”
“Maana
wakati huo hali ilikuwa mbaya sana, watu walikuwa wanapenda klabu zao
tu, hata wachezaji walikuwa hawataki kuchezea timu ya taifa, lakini
tukafanikiwa kuwarudisha na sasa imefikia mchezaji asipoteuliwa Taifa
Stars anaumia, hata klabu zinapenda wachezaji wao waitwe timu ya
taifa,”alisema Dk. Kikwete.
Rais
huyo mstaafu amewaomba Watanzania kujitokeza kwa wingi Jumamosi Uwanja
wa Taifa, kushangilia Taifa Stars ili kuwatia nguvu na hamasa wachezaji
wawafunge Algeria.

Hakuna maoni :