![]() |
Kilimanjaro
Stars inashiriki michuano hiyo mikongwe kabisa barani Afrika, ambapo
jumla ya nchi 12 wanachama wamedhibitisha kushiriki michuano hiyo
itakayomalizika Disemba 6 mwaka huu.
Nchi
zingine zinazoshiriki michuano hiyo ni tofati na Tanzania bara ni
Burundi, Djibouti, Ethiopia, Eritrea, Kenya, Rwanda, Somalia, Sudani,
Sudani Kusini, Uganda na Zanzibar.
Kibadeni
mshambuliaji wa zamani wa Simba SC, na timu ya Taifa Tanzania, ni kocha
mwenye leseni B, ambapo ameshafundisha vilabu vingi chini kwa mafanikio
ikiwemo kuifiksha klabu ya Simba katika hatua ya fainali ya kombe la
Washindi mwaka 1993.
Kocha
Kibadeni ni mkurugenzi wa ufundi wa kituo cha mchezo cha KISA kilichopo
Chanika, amewahi pia kuzifundisha timu za Kagera Sugar, JKT Ruvu.
Kocha
msaidizi wa Kilimanjaro Stars, Juma Mgunda ana leseni B ya CAF, zamani
alikuwa mshambuliaji wa timu ya Coastal Union na timu ya Taifa Tanzania,
pia aliweza cheza soka la kulipwa katika klabu ya Nahd nchini Oman.
Mgunda
amewahi kuifundisha timu ya Coastal Union ya jijini Tanga, timu ya mkoa
wa Tanga, kocha wa kituo cha vijana cha mkoa wa Tanga.
Aidha, Mgunda ni mkufunzi wa msaidizi wa mafunzo ya makocha ngazi pevu.


Hakuna maoni :