SIASA

SIASA

MAONI

MAONI

BURUDANI

MICHEZO

/ / KOCHA KERR WA SIMBA APAA ZAKE AFRIKA KUSINI AKISISTIZA SUALA LA MSHAMBULIAJI MCHANA NYAVU


Kocha wa Simba, Dylan Kerr ameondoka nchini kwenda Afrika Kusini huku akisisitiza kwamba anataka mshambuliaji mwenye uwezo mkubwa atakayeweza kusaidiana na Hamisi Kiiza kuipa Simba mabao.



Kocha huyo alikwea pipa jana Jumapili kwenda Sauz ikiwa ni safari binafsi lakini pia akiwa huko atapata fursa ya kuangalia uwezekano wa kupata fowadi aliyemlilia tangu mwanzoni mwa msimu huu, pamoja na beki wa kati atayesaidiana na Juuko Murshid na Hassan Isihaka.

Katika ripoti yake, Kerr alisema kuwa alipendekeza atafutiwe fowadi mmoja anayejua nyavu kwa ajili ya kusaidiana na Hamisi Kiiza, ambaye amekuwa ndiye jicho tangu kuanza kwa ligi kuu msimu huu akiwa na mabao nane.

Mratibu wa Simba, Abbas Ally, amesema kuwa, kocha huyo anatarajia kurejea Bongo Jumapili ijayo, tayari kuanza kwa mikakati ya kuikabili Azam katika mchezo wa Ligi Kuu Bara utakaopigwa Desemba 12, mwaka huu.

“Ni kweli kocha ameondoka leo (jana Jumapili) kwenda Sauz, anatarajia kurejea Jumapili wiki ijayo ili kuendelea na majukumu yake ya kikazi. Timu inatarajia kuanza mazoezi Novemba 16, kujiandaa na mchezo wetu dhidi ya Azam,” alisema Ally.

Ally hakutaka kuweka wazi iwapo Kerr ataangalia mchezaji anayeweza kumsajili kutoka huko lakini Championi Jumatatu linafahamu kuwa atakuwa akisaka straika pamoja na beki.


Simba inatajwa kumuwinda straika wa Vital’O, Laudit Mavugo lakini imetega macho yake sehemu nyingi ili kuweza kupata straika sahihi wa kutatua tatizo lao la ushambuliaji.

«
Next

Chapisho Jipya

»
Previous

Taarifa za zamani

About Unknown

Asante kwa kutembelea SELASINI HABARI,NITAKUHABARISHA, KUKUELIMISHA NA KUKUBURUDISHA HIVYO USIKOSE KUTEMBELEA SELASINIHABARI.BLOGSPOT.COM.

Hakuna maoni :

Leave a Reply