SIASA

SIASA

MAONI

MAONI

BURUDANI

MICHEZO

/ / KOCHA SIMBA AAMUA KUWATUNDIKA MDANTAONI ANAOWAITA WANAFIKI



Kocha Mkuu wa Simba, Muingereza, Dylan Kerr, amesema katika maisha amepitia mambo mengi na kukumbana na changamoto nyingi zilizomfanya akomae na bado anaendelea kukutana nazo.


Kauli hiyo imekuja siku chache baada ya kuandika ujumbe kupitia ukurasa wake katika akaunti ya Mtandao wa Kijamii ya Twitter kuwa: “Watu wanakuchekea kinafiki usoni mwako na wakiwa pembeni wanakusaliti.”

Alipotafutwa, kocha huyo ambaye alitibuana na waliokuwa wasaidizi wake, Mserbia, Dusan Momcilovic na Selemani Matola, ambapo alisema hakumlenga yeyote ila hali hiyo ni ya kawaida kutokea kwa mtu yeyote.


“Katika maisha kuna marafiki wa kawaida na wale mnaojuana kiundani, ndiyo nilikuwa namaanisha hivyo. Najua hata wewe umeshawahi kukutana na hali hiyo, hivyo basi unatakiwa kumuamini mtu mmoja tu, ambaye ni mama yako na si mwingine,” alifafanua Kerr bila kuelezea kiundani hasa.

«
Next

Chapisho Jipya

»
Previous

Taarifa za zamani

About Unknown

Asante kwa kutembelea SELASINI HABARI,NITAKUHABARISHA, KUKUELIMISHA NA KUKUBURUDISHA HIVYO USIKOSE KUTEMBELEA SELASINIHABARI.BLOGSPOT.COM.

Hakuna maoni :

Leave a Reply