SIASA

SIASA

MAONI

MAONI

BURUDANI

MICHEZO

/ / MAGURI, BOCCO WAPIGA MBILIMBILI STARS IKIIUA SOMALIA MABAO 4-0 CHALENJI


Washambuliaji Elias Maguri na John Bocco kila mmoja ametupia bao mbili na kuiwezesha Kilimanjaro Stars kushinda kwa mabao 4-0 dhidi ya Somalia.

Stars imeibuka na ushindi huo katika mechi yake ya kwanza ya michuano ya Chalenji nchini Ethiopia.

Bocco na Maguri walianza kufunga bao mojamoja katika kipindi cha kwanza, wakafanya hivyo katika kipindi cha pili.

Stars chini ya Abdallah Kibadeni inahitaji ushindi mwingine ili kusonga mbele na itakutana na Rwanda mechi itakayopigwa Jumanne.


Kikosi cha Kibadeni kipo Kundi A na timu za Ethiopia, Somalia na Rwanda.

«
Next

Chapisho Jipya

»
Previous

Taarifa za zamani

About Unknown

Asante kwa kutembelea SELASINI HABARI,NITAKUHABARISHA, KUKUELIMISHA NA KUKUBURUDISHA HIVYO USIKOSE KUTEMBELEA SELASINIHABARI.BLOGSPOT.COM.

Hakuna maoni :

Leave a Reply