SIASA

SIASA

MAONI

MAONI

BURUDANI

MICHEZO

/ / WA ZAMANI CHELSEA ADAI SASA COSTA HANA MPIRA NI UBABE TU!


costa 0Beki wa zamani wa Chelsea Frank Sinclair amemshambulia Straika wa Klabu hiyo Diego Costa kuwa Msimu huu amedorora kwa sababu amepania kuonyesha ubabe badala ya kucheza Mpira.
Msimu uliopita, Costa ambae ni Mzaliwa wa Brazil alieamua kuichezea Spain, aliifungia Chelsea Mabao 20 na kukisaidia Kikosi cha Jose Mourinho kutwaa Ubingwa wa Ligi Kuu England pamoja na Kombe la Ligi.
Lakini Msimu huu, yeye na wenzake wamedorora na kuwa goigoi kiasi cha yeye kufunga Bao 2 tu katika Mechi 12 za Ligi na kuifanya Chelsea itupwe Nafasi ya 16 kwenye Ligi.
Msimu huu Costa, ambae kawaida ni mkorofi Uwanjani, amezidisha ukorofi wake na kufungiwa mara 2 na Juzi Jumamosi Chelsea walipofungwa 1-0 na Stoke City Mchezaji huyo alionekana kugombana kila mara na Sentahafu wa Stoke Ryan Shawcross.
Akihojiwa kuhusu hali tete ya Klabu yake ya zamani Chelsea, Frank Sinclair, alieleza: "Tatizo kubwa ni Costa kupania kuonyesha ubabe badala ya kucheza Mpira kama alivyofanya Msimu uliopita!"
Sinclair amesema Msinu huu kila mbinu ya Costa kuwazidi akili Mabeki imeshindwa na sasa amebaki kuonyesha utemi tu Uwanjani.

«
Next

Chapisho Jipya

»
Previous

Taarifa za zamani

About Unknown

Asante kwa kutembelea SELASINI HABARI,NITAKUHABARISHA, KUKUELIMISHA NA KUKUBURUDISHA HIVYO USIKOSE KUTEMBELEA SELASINIHABARI.BLOGSPOT.COM.

Hakuna maoni :

Leave a Reply