Zambia,
Uganda, Congo DR, Morocco na Guinea zimeungana na Gabon kutinga hatua
ya Makundi ya kuwania Nafasi 5 za Afrika kwenye Fainali za Kombe la
Dunia za Mwaka 2018 huko Russia.Juzi Gabon ilikuwa Nchi ya kwanza kutinga hatua hiyo baada ya kuifunga Mozambique 1-0 huko Libreville katika Mechi ya Marudiano na hivyo kufungana baada ya wao kufungwa 1-0 katika Mechi ya kwanza na wao kupenya kwa Mikwaju ya Penati 4-3.
Uganda, ambao waliifunga Togo 1-0 Ugenini katika Mechi ya kwanza, Jana wakiwa kwao Nakivubo waliitwanga Togo 3-0 na kufuzu huku Bao za0 2 zikifungwa na Kijana wa Miaka 17, Farouk Miya, na jingine kufungwa na Kepteni Geoffrey Massa.
Nao Zambia, maarufu kama Chipolopolo, Jana huko Ndola waliitwanga Sudan 2-0 na kufuzu Makundi kwa Jumla ya Mabao 3-0 huku Bao zao hiyo Jana zikifungwa na Lubambo Musonda na Winston Kalengo.
Congo DR Jana walitoka 2-2 na Burundi huko kwao lakini wamesonga baada ya kushinda Mechi ya kwanza 3-2 huko Bujumbura.
Morocco nao wamefuzu licha ya Jana kufungwa 1-0 na Equatorial Guinea baada ya wao kushinda Mechi ya kwanza 2-0.
Guinea, wakiutumia Uwanja wa Mjini Casablanca, Morocco kama Uwanja wa Nyumbani, waliifunga Namibia 2-0 na kusonga kwa jumla ya Mabao 3-0.
Timu hizi 6 zilizofuzu zitaungana na Nchi nyingine 14 zitakazofuzu Jumanne na kupangiwa Makundi Matano ya Timu 4 kila moja na Mshindi wa kila Kundi kutinga kwenye Fainali za Kombe la Dunia za Mwaka 2018 huko Russia.
KOMBE LA DUNIA 2018
RATIBA/MATOKEO:
Afrika-Raundi ya Pili
Marudiano
**Saa za Bongo
Jumapili Novemba 15
Zambia 2 Sudan 0 [Jumla ya Mabao Mechi Mbili: 3-0]
Uganda 3 Togo 0 [4-0]
Congo, DR 2 Burundi 2 [5-4]
Equatorial Guinea v Morocco [1-0]
Guinea 2 Namibia 0 [3-0]
Jumanne Novemba 17
[Kwenye Mabano Matokeo Mechi za Kwanza]
16:30 Rwanda v Libya (0-1)
17:00 Cameroon v Niger (3-0)
17:30 Congo v Ethiopia (4-3)
18:00 Ghana v Comoros (0-0)
18:00 Nigeria v Swaziland (0-0)
19:30 Egypt v Chad (0-1)
20:00 Tunisia v Mauritania (2-1)
20:00 South Africa v Angola (3-1)
20:00 Ivory Coast v Liberia (1-0)
21:00 Burkina Faso v Benin (1-2)
21:15 Algeria v Tanzania (2-2)
22:00 Cape Verde v Kenya (0-1)
22:00 Senegal v Madagascar (2-2)
22:00 Mali v Botswana (1-2)
**Washindi kutinga hatua ya Makundi

Hakuna maoni :