Hungary
imefanikiwa kutinga Fainali za Mataifa ya Ulaya, EURO 2016, baada ya
kuifunga Norway 2-1 katika Mechi ya Mchujo hapo Jana na hii ni mara ya
kwanza kwao kucheza Fainali za Mashindano makubwa tangu 1986.Ushindi huo umewafanya wafuzu kwa Jumla ya Mabao 3-1 kwa Mechi mbili baada ya pia kushinda Mechi ya kwanza Ugenini kwa Bao 1-0.
Hapo Jana Bao za Hungary zilifungwa na Tamas Priskin na Markus Henriksen aliejifunga mwenyewe huku Bao la Norway likifungwa na huyo huyo Markus Henriksen.
Mechi nyingine 3 za Mchujo zitachezwa Jumatatu na Jumanne.
Washindi Wanne wa Mechi hizi wataungana na Nchi nyingine 20 ambazo zimeshafuzu, wakiwamo Wenyeji France, na kufanyiwa Droo Mwezi Desemba kupanga Makundi na Ratiba ya Fainali za EURO 2016.
TIMU ZILIZOFUZU [20 bado 4-Zitatoka Mechi 4 za Mchujo]:
-France [Wenyeji]
-KUNDI A: Iceland, Czech Republic, Turkey
-KUNDI B: Belgium, Wales
-KUNDI C: Spain, Slovakia
-KUNDI D: Germany, Poland
-KUNDI E: England, Switzerland
-KUNDI F: Northern Ireland, Romania
-KUNDI G: Austria, Russia
-KUNDI H: Italy, Croatia
-KUNDI I: Portugal, Albania
Fainali za EURO 2016 zitachezwa Mwakani kuanzia Juni huko France.
EURO 2016
Mechi za Mchujo
Ratiba/Matokeo:
Marudiano
**Saa za Bongo
Jumapili Novemba 15
[Kwenye Mabano Jumla ya Mabao kwa Mechi Mbili]
Hungary 2 Norway 1 [3-1]
[Kwenye Mabano Matokeo Mechi za Kwanza]
Jumatatu Novemba 16
22:45 Ireland v Bosnia And Herzegovina [1-1]
Jumanne Novemba 17
22:45 Slovenia v Ukraine [0-2]
22:45 Denmark v Sweden [1-2]

Hakuna maoni :