SIASA

SIASA

MAONI

MAONI

BURUDANI

MICHEZO

/ / LICHA YA KUWA MPINZAJI AKIWA NA PSG, ZLATAN AKARIBISHWA NA JINA LAKE JUU YA GHOROFA


 Wakati Zlatan Ibrahimovic anarejea katika mji aliokulia wa Malmo, safari hii akiwa mpinzani, wadau wameamua kuonyesha heshima kwake kwa kumkaribisha kwa mfumo wa aina yake.


Jengo refu kuliko yote katika mji wa Malmo m nchini Sweden limepambwa kwa herufi kubwa ya Z ikiwa na maana Zlatan.


Zlatan ameshatua Malmo akiwa na PSG ya Ufaransa ambayo inacheza na timu hiyo Ligi ya Mabingwa Ulaya leo usiku.

Zlatan amewaambia  mashabiki wa Malmo wanaweza kuimba jina lake kama walivyokuwa wakifanya awali wakati akiitumikia timu hiyo.

Malmo ndiyo ilikuwa timu yake ya kwanza kubwa iliyomkuza kisoka kabla ya kununuliwa na Ajax ya Uholanzi.

Hajawahi kurejea na kucheza Malmo akiwa na timu kubwa kama PSG, hii ni mara yake ya kwanza.

Zlatan mwenye asili ya Yugoslavia alizaliwa katika kitongoji cha Rosenbarg mjini Malmo.

«
Next

Chapisho Jipya

»
Previous

Taarifa za zamani

About Unknown

Asante kwa kutembelea SELASINI HABARI,NITAKUHABARISHA, KUKUELIMISHA NA KUKUBURUDISHA HIVYO USIKOSE KUTEMBELEA SELASINIHABARI.BLOGSPOT.COM.

Hakuna maoni :

Leave a Reply