Aliyekuwa mgombea wa urais wa tiketi ya Chadema, Edward Lowassa
anatarajiwa kupanda jukwaani Jumamosi kumuombea kura mgombea wa ubunge
wa Chadema Jimbo la Arusha Mjini, Godbless Lema.
Akizungumza katika mkutano wa uzinduzi wa kampeni za ubunge katika jimbo
hilo uliofanyika Soko Kuu jana, Lema alisema Lowassa atazungumza na
Watanzania na kuwashukuru pia kwa kura nyingi walizompa.
Awali, mbunge mteule wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ alieleza
kuwa Lowassa na viongozi wa Chadema watatoa tamko zito siku hiyo na
kuwataka wakazi wa Arusha na Watanzania kutega masikio.
Lema ambaye pia ni mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, aliwataka wakazi wa
Arusha, kutokatishwa tamaa na kuendelea kuwa na huzuni kutokana na
matokeo ya urais yaliyotangazwa na kuwa bado kuna harakati za chama
hicho kusaka haki.
“Ndugu zangu msikate tamaa, tumesikia wengine wametupa shahada zao,
hapana, kazi ndiyo imeanza na lolote linaweza kutokea kwa uwezo wa
Mungu,” alisema.
Alisema huzuni ya matokeo yaliyotangazwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi
(NEC), haipo kwa wananchi tu, bali hata wajumbe wote wa kamati kuu.
“...Kwenye kikao cha kamati kuu, kuna wajumbe walimuomba Lowassa atoe
tamko... kama angetoa tamko la kupinga matokeo na kukubali watu kuingia
mitaani, Tanzania ingekuwa imeingia katika machafuko makubwa.
“Tunaendelea kutumia taasisi za kimataifa kudai haki, ndiyo sababu
mnaona Zanzibar wameshindwa kujitangazia matokeo, hii ni kazi kubwa ya
Ukawa,” alisema.
Katika mkutano huo, Lema alieleza njama alizosema zinapangwa kumnyima
ushindi na akaonya kuwa hatakuwa tayari kuona ameshinda lakini mwingine
akatangazwa kushinda.
“Najua Arusha nitashinda kwa kura nyingi, lakini kama wakitaka kunipora ushindi sitakubali,” alisema Lema.
Aliwaomba wakazi wa Arusha kujitokeza kwa wingi Desemba 13 kumpigia kura
nyingi, ili pia kuwezesha Chadema kupata viti viwili zaidi vya wabunge
wa viti maalumu.
Home
/
SIASA
/
Lowassa kumnadi Godbless Lema Arusha Mjini Jumamosi hii....Pia Atalitumia Jukwaa Hilo Kuwashukuru Watanzania
Lowassa kumnadi Godbless Lema Arusha Mjini Jumamosi hii....Pia Atalitumia Jukwaa Hilo Kuwashukuru Watanzania
Tagged with: SIASA


Hakuna maoni :