MKUU wa Wilaya ya Kinondoni Paul Makonda kwa kushirikiana na kampuni ya
Push Mobile leo wamezindua mfumo mpya wa utoaji taarifa ya uzembe
unaofanyika katika sekta muhimu zilizopo wilayani humo.
Huduma hiyo itawahusu wananchi waishio Wilaya ya Kinondoni tu. Wananchi
hao watapata fursa ya kutuma ujumbe kwa njia ya simu ya mkononi ambao
utamfikia Makonda moja kwa moja na hivyo kumwezesha kushughulikia kero
husika.
Akizungumza na waandishi wa habari leo ofisini kwake Jijini Dar es
Salaam, Makonda amesema, wananchi wanatakiwa kutoa taarifa kuhusu kero
za huduma muhimu kuanzia tiba mahospitalini, usafiri barabarani,
mahakamani, masuala ya ardhi, polisi na maeneo ya biashara.
“Kwa mfano mtu uko eneo la biashara au uko katika kituo cha polisi
umekaa kwa muda mrefu hakuna huduma, ukiuliza unajibiwa vibaya, au upo
mahakamani kesi yako inazungushwa kwa muda mrefu mahakimu hawapo.
Kuanzia hapo hapo ulipo unaweza kutuma malalamiko yako kwa kuandika neno
‘Kinondoni’ kisha unaacha nafasi, halafu unaandika kero yako kwa kifupi
kwenda namba 15404. Ujumbe huo utanifikia moja kwa moja nami nitachukua
hatua stahiki,” amesema Makonda.
“Nimewaandaa vijana wangu wasiopungua watano ambao nitafanya nao kazi
watakuwa wakipokea ujumbe kutoka kwa wananchi na kuweza kutambua kama ni
ukweli au uongo. Tutamtambua mtu huyo aliyetuma ujumbe eneo alipo kwa
kutumia kompyuta zilizounganishwa kwenye mitambo maalumu na kisha
tutafuatilia”. Amesema Makonda.
Makonda alisema kwamba, mkakati huo utakuwa ni endelevu ambapo wananchi
wa Kinondoni watatuma ujumbe kwa masaa 24. Mkakati huu umepewa jina la
“Sukuma twende”.
“Kila wiki nitakuwa nakutana nafanya tathmini
ili kuangalia ni sekta ipi imelalamikiwa sana. Ikionekana ipo iliyobeba
kero nyingi nitawaandikia barua za onyo, au kuagiza watumishi
wabadilishwe vitengo kwa kupelekwa hata kijijini, kama sio kuwafukuza,” amesema Makonda.
Home
/
SIASA
/
Makonda Afuata Nyayo za Dk John Magufuli Azindua ‘Sukuma Twende’ Kinondoni Kuwakomesha Watendaji Wabovu wa Serekali
Makonda Afuata Nyayo za Dk John Magufuli Azindua ‘Sukuma Twende’ Kinondoni Kuwakomesha Watendaji Wabovu wa Serekali
Tagged with: SIASA


Hakuna maoni :