Tarehe 27 mwezi May, mwaka 2014 siku ya Jamanne majira ya saa 4 asubuhi,
kwenye kipindi cha maswali na majibu, Naibu waziri wa habari vijana,
utamaduni na michezo Juma Nkamia alieleza makadirio ya gharama za
kukimbiza Mwenge wa Uhuru nchini.
Nkamia alisema "serikali kuu hutenga kiasi cha fedha kulingana na
mahitaji na gharama halisi ya wakati husika.. Mwaka 2012 jumla ya
shilingi Bilioni 43 zilitumika ambapo kati ya hizo Bilioni kumi na moja
(11) zilitengwa na serikali na Bilioni 32 zilichangwa na mashirika,
taasisi, makampuni na wadau mbalimbali walioombwa kuchagia kwa ajili ya
kuadhimisha uzinduzi na kilele cha mbio za mwenge wa uhuru." Taarifa
zinaonesha kuwa mwaka 2014 inakadiriwa jumla ya Shilingi Bilioni 120
zilitumika kama gharama ya kukimbiza Mwenge nchi nzima.
CALCULATION.
Bilioni 120 zinazotumika kukimbiza mwenge nchini (mwaka huu huenda zikaongezeka), zinatosha kufanya yafuatayo;
1. Kununua mashine 60 za MRI na CT Scan kwa ajili ya kuhudumia wagonjwa
wenye kuhitaji vipimo hivyo. Ikumbukwe hospitali ya Taifa ya Muhimbili
kuna mashine moja tu ya MRI na moja ya CT Scan ambazo zote ni mbovu.
Fedha za Mwenge zinaweza kununua mashine 60 za aina hiyo.
Rais Magufuli alijaribu kuhimiza ukarabati wa mashine hizo lakini
zilifanya kazi kidogo tu kisha zikafa tena. Kwa sasa hakuna huduma za
Vipimo vya MRI Hospitali ya Muhimbili, hadi imefikia hatua wagonjwa
wametunga kirefu cha MRI kuwa ni;
-Magufuli -Rudi -Imeharibika tena.
2. Shilingi Bilioni 120 zinazotumika kukimbiza Mwenge zinatosha kulipia
mikopo ya wanafunzi 61,624 wa vyuo vya Elimu ya Juu nchini. Hadi sasa
takribani wanafunzi 40,000 walioko vyuoni hawajapata mikopo. Kumbe fedha
za Mwenge zingeweza kuwalipia mikopo wanafunzi wote waliobaki na
chenchi ikabaki (61624 -40000) x 1,960,000 = 4,238,304,000. Ikabaki
chenchi ya Bilioni 4.2
3. Bilioni 120 za Mwenge zinatosha kujenga Zahanati 3,870 kwa gharama ya
Mil.41 kila Zahanati. Kwa mujibu wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi mwaka huu
Tanzania ina jumla ya Kata 3,802. Kwahiyo Bil.120 za Mwenge zinatosha
kujenga Zahanati kila Kata nchini na chenchi ikabaki. (3870-3802) ×
41,000,000 = 2,788,000,000. Ikabaki chenchi ya Bilioni 2.7
4. Bil 120 za Mwenge zinatosha kununua Boti 13 za kisasa za majini kama
ile ya Bakharesa (Kilimanjaro 5). Ikumbukwe ukiondoa boti za Bakhresa,
serikali haina usafiri wa kueleweka wa kwenda Zanzibar. Meli mbili za
Mv. Spice Islanders na Mv.Scagget zilizama na kuua maelfu ya watanzania
kutokana na uchakavu wa meli hizo. Kwahiyo Bil.120 za Mwenge zingeweza
kununua meli mpya za kisasa kwa ajili ya usafiri wa Zanzibar na nchi
jirani ktk bahari ya Hindi kama Msumbiji, Comoro na Kenya. Hii ingekua
njia ya kuongeza pato la taifa kupitia sekta ya usafiri majini.
On other hand tungenunua Boti za kisasa tungeweza kupromote utalii wa
fukwe (Beach Tourism). Nchi ya Mauritius inaingiza zaidi ya Shilingi
Trilioni 10 kwa mwaka (nusu ya bajeti ya Tanzania) kupitia utalii wa
fukwe tu. Mauritius hawana Mbuga za wanyama, hawana mlima mrefu kama
Kilimanjaro, lakini wanapata Trilioni 10 kwa mwaka kupitia utalii wa
fukwe, Tanzania tuna vivutio vya kila aina lakini tunaingiza Trilioni
1.7 tu kupitia sekta ya utalii.
Kwahiyo tukitumia fedha za Mwenge tunaweza kuboresha utalii wa fukwe na
kuvutia watalii wengi zaidi na kupata mapato makubwa zaidi kutokana na
sekta ya utalii.
5. Bil 120 za Mwenge zikikusanywa kwa miaka mitano (120 bil x 5 = 600
Bil) zinatosha kununua Ndege kubwa za kisasa zipatazo 10 angalau na sisi
tukawa na Shirika letu la ndege. Kwa mujibu wa mtandao wa
www.aircraftcompare.com bei ya ndege aina ya Boeing 737 yenye uwezo wa
kubea abiria 240 ni USD 43 Million sawa na Shilingi za kitanzania
Bil.80.
Kwahiyo Bil.600 za Mwenge (kwa miaka mitano) zinaweza kununua ndege kama
10 hivi angalau na sisi tukafufua Air Tanzania yetu tukaanza kushindana
na Kenya Airways, Rwandan Air au Ethiopian Airways.
Kwa ujumla yako mambo mengi sn fedha za Mwenge zinaweza kufanya ikiwa
zitatumiwa vzr. Hizi nilizotoa ni alternatives chache tu lakini kama
viongozi wetu wakiwa makini wanaweza kufanya makubwa zaidi ya haya.
Written By Malisa GJ
Home
/
MATUKIO
/
Magufuli Tafadhali Tuondolee Mbio za Mwenge, Hazina Faida Kwa Taifa zaidi ya Kutafuna Mabilioni Kila Mwaka
Magufuli Tafadhali Tuondolee Mbio za Mwenge, Hazina Faida Kwa Taifa zaidi ya Kutafuna Mabilioni Kila Mwaka
Tagged with: MATUKIO
Hakuna maoni :