SIASA

SIASA

MAONI

MAONI

BURUDANI

MICHEZO

/ / MAN UNITED NDIO KINARA KUTOA WACHEZAJI WENGI WA KIMATAIFA ULAYA!


MANUNITED-CARRINGTONManchester United ndio inaongoza kwa kutoa Wachezaji wengi wa Kimataifa kwa huko England na pia Barani Ulaya.

Msimu huu, Wachezaji wengi wameteuliwa kuzichezea Timu zao za Taifa na Wachezaji wanaocheza Ligi Kuu England ndio wanaongoza kwa Ulaya huku Man United wakiwa juu kwa kutoa Wachezaji wengi zaidi.

Kwa mujibu wa Takwimu za CIES Football Observatory Digital Atlas, Asilimia 41 ya Wachezaji waliocheza Ligi Kuu England Msimu huu wamechezea pia Timu zao za Taifa Msimu huu huu.

Man United wapo juu kwa kutoa Wachezaji Asilimia 72 ya wale walioteuliwa na Meneja wao Louis van Gaal kucheza Mechi za Ligi Kuu England Msimu huu ambao pia waliteuliwa kucheza Timu zao za Taifa.

Ijumaa iliyopita, Wachezaji wa Man United waliovaa Jezi za Nchi zao ni Michael Carrick, Phil Jones, Chris Smalling, Wayne Rooney na Juan Mata ambao walicheza wakati Spain inaichapa England 2-0, wakati Anthony Martial na Morgan Schneiderlin walikuwa kwenye France iliyoichapa Germany ambayo ilikuwa nayo Bastian Schweinsteiger huku Daley Blind akiichezea Netherlands na Matteo Darmian akiichezea Nchi yake Italy.
KLABU ENGLAND-Asilimia za Wachezaji wa Kimataifa:
1
Manchester United
72.0
2
Chelsea
66.7
3
Arsenal
64.0
-
Tottenham
64.0
5
Manchester City
51.9
6
Liverpool
50.0
7
Southampton
44.4
8
West Brom
43.5
9
Swansea City
40.0
10
Everton
39.3
-
Crystal Palace
39.3
12
Stoke City
38.5
-
Leicester City
38.5
14
Norwich City
34.6
15
Bournemouth
33.3
16
Watford
27.6
-
Sunderland
27.6
18
Newcastle
25.0
19
Aston Villa
22.2
20
West Ham
20.0
KLABU ULAYA-Asilimia za Wachezaji wa Kimataifa:
1
Manchester United
72.0
2
CSKA Moscow
71.4
3
Real Madrid
69.6
4
Chelsea
66.7
5
Arsenal
64.0
-
Tottenham
64.0
7
PSG
63.6
8
Juventus
60.0
9
Atletico Madrid
57.1
10
Dynamo Kiev
56.0
-
Barcelona
56.0

«
Next

Chapisho Jipya

»
Previous

Taarifa za zamani

About Unknown

Asante kwa kutembelea SELASINI HABARI,NITAKUHABARISHA, KUKUELIMISHA NA KUKUBURUDISHA HIVYO USIKOSE KUTEMBELEA SELASINIHABARI.BLOGSPOT.COM.

Hakuna maoni :

Leave a Reply