HALI isiyokuwa ya kawaida Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza, limekiuka
sheria na kuanza kupiga mabomu ya macho katika Hospitali ya Rufaa ya
Bugando (BMC), kuwatawanya wafuasi wa Chadema. Anaandika Moses Mseti, Mwanza … (endelea).
Tukio hilo limetokeaza leo jioni, baada ya wafuasi hao kuanza mvutano na
askari Polisi mmoja na ndipo vurugu zilizodumu kwa saa moja na nusu.
Hata hivyo wafuasi hao kabla ya kuanza vurugu hizo, walizima kuruka kuta za hospitali na kufungua geti kwa mabavu.
MwanaHALISI Online ilishuhudia Polisi huyo na wafuasi wa Chadema wakivutana nje ya mlango wa vyumba vya kuhifadhi maiti.
Baada ya mvutano huo wafuasi hao wa Chadema walianza kumuangushia
kichapo askari huyo ambaye anatuhumiwa kufanya njama za kurudisha mwili
wa marehemu mkoani Geita kwa madai kwamba tukio lilitokea huko.
Hali hiyo ya askari kuangushiwa kichapo, lilikuja gari la polisi ambalo
lilikuwa na polisi ambao walikuwa na mabomu ya machozi na silaha za moto
na kuanza kipiga mabomu.
Aidha Mwandishi wa habari hizi, alishuhudia Polisi mmoja akimpiga mjane
wa marehemu, katika vurugu hizo ambazo zilianzishwa na polisi wenyewe
ambao walilazimisha kuingia kwenye chumba hicho.
Katika vurugu hizo, polisi walimtia mbaroni Mwenyekiti wa Bavicha Taifa, Pastrobas Katambi na baadhi ya wafuasi zaidi ya wanne.
Awali wakati wafuasi wa Chadema wakiupokea mwili wa marehemu, walikuwa
walisikika wakiimba, “Kama sio wewe Mkapa na mauaji yangetoka wapi.”
Hata hivyo wafuasi hao ambao waliupokea mwili wa marehemu katika kivuko
cha Busisi ambapo walipofika kati kati ya Jiji la mwanza walitokea
wafuasi wengine ambao walikuwa nao walisikika wakiimba,” CCM wameua CCM
wameua… Hadi katika BMC.
Kifo cha Mawazo kinahusishwa na mmoja wa viongozi wakubwa wa CCM Mkoa wa
Geita, ambaye ni mmiliki wa mabasi yanayofanya safari zake Mwanza –
Geita.
Kuhusishwa kwa kigogo huyo wa CCM na kifo hicho, inadaiwa kuwa gari lake
lilionekana likiwabeba vijana wanaotajwa kuhusika na mauaji hayo na
kuwaleta mjini hapa.
Pia kigogo huyo ambaye ni Mbunge mteule wa kati ya majimbo ya mkoa huo,
anahusishwa kuandaa mtandao wa wauaji hao ambao mmoja wao anadaiwa
kutoka jijini hapa.
Pia Mawazo ambaye alikuwa ni mgombea ugunge jimbo la Busanda akichukuana
na Lolencia Bukwimba (CCM) inadaiwa alikuwa anatarajiwa kwenda
mahakamani kupinga ushindi wa Bukwimba.
Hata hivyo inaelezwa kuwa endapo kama marehemu angefungua mashtaka
polisi angeshinda kesi kutokana na ushahidi wa video zinazowaonesha
polisi kuwatisha mawakala wa Chadema kusaini matokeo kwa lazima.
Akizungumza na wafuasi wa Chadema, Godbless Lema, amesema kifo cha
Mawazo ni mpango wa Chama cha Mapinduzi na kuitaka Jeshi la Polisi
kuwakamata watu wanaohusishwa na kifo hicho.
Source:Mwanahalisi
Tagged with: MATUKIO

Hakuna maoni :