Rais wa Marekani Barack Obama ameipa
Afrika ya Kusini siku 60 kuondoa vikwazo katika bidhaa za kilimo kutoka
Marekani la sivyo ataiondolea msamaha wa kodi wa bidhaa.
Obama amechukua hatua hiyo kwa vile Afrika Kusini imeendelea kuweka vikwazo kwa wafanyabiashara wa Marekani.
Afrika Kusini imepiga marufuku kuagiza mazao ya kuku mwezi Decemba kutokana na kutokea kwa mlipuko wa ugonjwa wa mafua ya ndege na kwa miaka kadhaa imekuwa ikitoa adhabu ya kodi kwa baadhi ya bidhaa za kuku kutoka Marekani.
Hakuna maoni :