SIASA

SIASA

MAONI

MAONI

BURUDANI

MICHEZO

/ / Platini apigwe marufuku ya maisha :FIFA

Kamati ya maadili ya FIFA imependekeza kuwa rais aliyesimamishwa kazi wa UEFA Michel Platini apigwe marufuku ya maisha asishiriki maswala yeyote ya kandanda.
Wakili wake ameiambia shirikisho la habari la AFP kuwa kamati ya nidhamu ilikuwa imependekeza marufuku ya maisha kwa mteja wake kufuatia malipo ya mamilioni ya Euro kwa kazi ambayo yadaiwa alimfanyia rais wa shirikisho la soka duniani ambaye pia amepigwa marufuku Sepp Blatter.
Platini na Blatter wote wanatumikia marufuku ya siku 90 kufuatia uchunguzi wa malipo ya dola milioni mbili.
Wakili anayemwakilisha Platini, Thibaud d'Ales ametaja kauli hiyo kuwa inayozidi mipaka.






''Kwa hakika marufuku hii bado hata haijathibitishwa kuwa kweli ilikuwa ni ufisadi ilhali mteja wangu anapendekezwa kupigwa marufuku ya maisha?''
''Haina msingi wowote kisheria'' alidai D'Ales
Wawakilishi wa rais Sepp blatter walikataa kuthibitisha kuwa walikuwa wamepokea mapendekezo sawa na hayo.
Kamati ya nidhamu ya FIFA ilipendekeza jumatatu kuwa Blatter na Platini wafunguliwe mashtaka ya ufisadi na ubadhirifu wa mali ya FIFA.





Kauli yake hata hivyo itatangazwa reasmi mwezi ujao na hadi hapo itakapotoa msimamo wake Platini hatoruhusiwa kuwania urais wa shirikisho la soka duniani FIFA.

Platini ni miongoni mwa wagombea 5 wanaotaka kumrithi rais wa shirikisho hilo Sepp Blatter katika uchaguzi unaotarajiwa kufanyika mwezi Februari mwakani.
Wakili wake anadai huenda ni njama ya kumshurutisha Platini asiwanie uongozi wa FIFA katika uchaguzi ujao.

«
Next

Chapisho Jipya

»
Previous

Taarifa za zamani

About Unknown

Asante kwa kutembelea SELASINI HABARI,NITAKUHABARISHA, KUKUELIMISHA NA KUKUBURUDISHA HIVYO USIKOSE KUTEMBELEA SELASINIHABARI.BLOGSPOT.COM.

Hakuna maoni :

Leave a Reply