Rais
wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF), Jamal Malinzi amewatumia
salamu za pongezi wachezaji Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu
wanaochezea klabu ya TP Mazembe ya Congo DR kufuatia kutwaa Ubingwa wa
Ligi ya Mabingwa Afrika (CL) jana kwa kuifunga timu ya USM Algiers kwa
jumla ya mabao 4-1.
Katika salamu zake kwenda kwa wachezaji hao, Malinzi amewapa
hongera kwa mafanikio waliyofikia ya kutwaa ubingwa huo wa vilabu
Afrika, na kuwataka waongeze bidii ili waweze kufanya vizuri pia katika
michuano ya Kombe la Dunia la Mabara litakalofanyika mwezi Disemba
nchini Japan.
Malinzi amesema kwa niaba ya familia ya mpira wa miguu na
Watanzania wote wanawashukuru kwa kuiwakilisha vizuri Tanzania
kimataifa, na sasa moyo huyo wa kujituma kwao waundeleleze katika mchezo
dhidi ya Algeria wikiendi hii kuwania kufuzu kwa fainali za kombe la
Dunia 2018 nchini Urusi.
[09/11 11:33] Storming Fo: LEO UZINDUZI AZAM HD FEDERATION CUP!
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi
anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa michuano ya Kombe la
Shirikisho (AzamHD Federation Cup) utakaofanyika leo Jumatatu, saa 9
kamili mchana katika uwanja wa Karume ambapo timu ya Abajalo FC itacheza
dhidi ya Transit Camp zote za jijini Dar es salaam.
Michuano hiyo ilianza kutimua vumbi jana kwa mchezo mmoja kuchezwa
katika uwanja wa Karume uliopo mjini Musoma, ambapo Vill Squad ya jijini
Dar es salaam iliweza kuibuka na ushindi wa mabao 3- 1 dhidi ya timu ya
JKT Rwamkoma ya mkoani Kagera.
Katika uwanja wa CCM Kirumba, Pamba FC ya jijini humo watakua
wenyeji wa timu ya wachimba dhahabu kutoka mkoani Shinyanga, Bulyanhulu
FC mchezo utakaoza saa 10:30 jioni.
Jumla ya timu 64 zinashiriki michuano hiyo kutoka Ligi Kuu, Ligi
Daraja la Kwanza na Ligi Daraja la Pili kuwania kutwaa ubingwa, ambapo
Bingwa wa michuano AzamHD Federation Cup atapata nafasi ya kuwakilisha
nchi kwenye Kombe la Shirikisho barani Afrika mwaka 2017.
Hakuna maoni :