Upande wa Jamhuri katika kesi inayomkabili mwanafunzi wa Taasisi ya
Teknolojia Tanzania (DIT), Benedict Ngonyani, anayetuhumiwa kusambaza
taarifa katika mtandao wa kijamii wa Facebook kuwa Mkuu wa Jeshi la
Wananchi Tanzania (JWTZ), Jenerali, Davis Mwamunyange, amelishwa sumu,
umewasilisha mahakamani kusudio la kukata rufaa kupinga mshtakiwa huyo
kupewa dhamana.
Mwishoni mwa wiki iliyopita, Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar
es Salaam, iliyoketi chini ya Hakimu Mkazi Mkuu, Respicious Mwijage,
ilitengua hati ya kuzuia dhamana dhidi ya mshtakiwa huyo iliyowasilishwa
na Mkurugenzi wa Mashitaka Nchini (DPP).
Kabla ya uamuzi huo, hakimu alisikiliza hoja za mawakili wa pande zote
mbili na alikubaliana na maombi ya utetezi ya kumpa dhamana kwa kuwa
sababu za DPP kuzuia dhamana hiyo hazikuwa na msingi wa kisheria.
Wakili wa Serikali Mkuu, Theophil Mutakyawa aliwasilisha kusudio hilo
jana saa 7:00 mchana, kwamba upande wa Jamhuri haujaridhika na uamuzi wa
mahakama kutengua hati ya DPP.
Pia, kupitia kusudio hilo, upande wa Jamhuri unapinga Mahakama ya Kisutu
kutengua hati hiyo na kwamba haina mamlaka ya kuoindoa kwa kuwa
huondolewa na DPP ama kesi inapomalizika na kutolewa hukumu.
Awali hakimu alisema mshtakiwa ni mwanafunzi na shtaka analoshtakiwa
nalo linadhaminika kwa hiyo haoni haja ya kukosa masomo yake ya darasani
Katika kesi hiyo, inadaiwa Septemba 25, mwaka huu, jijini Dar es Salaam,
mshtakiwa alisambaza taarifa za uongo kinyume cha Sheria ya Makosa ya
Mtandao kifungu cha 16 ya mwaka 2015 kuwa Jenerali Mwamunyange
amenyweshwa sumu.
Home
/
MATUKIO
/
Sakata la Mkuu wa Majeshi Kulishwa Sumu: Serikali Yakata Rufaa Kupinga Mshitakiwa Kupewa Dhamana
Sakata la Mkuu wa Majeshi Kulishwa Sumu: Serikali Yakata Rufaa Kupinga Mshitakiwa Kupewa Dhamana
Tagged with: MATUKIO


Hakuna maoni :