MKONGWE wa siasa ambaye aliyekuwa Spika wa bunge la tisa, Samuel Sitta
ambaye alikuwa wakiwania nafasi ya uspika katika Bunge la 11, Kamati Kuu
ya (CCM) imelikata rasmi jina lake licha ya kufanya kampeni mapema juzi
kwenye viwanja vya Bunge.
Akitangaza majina yaliyopitishwa na kamati kuu Katibu wa Itikadi na
Uenezi, Nape Nnauye amesema katika halmashauri hiyo imeyapitisha majina
matatu ambayo ni Job Ndugai, Abdullah Ally Mwinyi na Tulia Akson.
Nape amesema kesho saa nne asubuhi majina hayo yatapelekwa yawasilishwa
kwa wabunge wa CCM kwa ajili ya kupitisha jina la mgombea mmoja ambaye
atagombea nafasi hiyo na wakambi ya upinzani.
Tagged with: SIASA


Hakuna maoni :