Taarifa inatolewa kwa wapenzi, mashabiki, wafuasi na wanachama wa
CHADEMA, wanaUKAWA na umma wa Watanzania wote wapenda mabadiliko kwa
ujumla kuhusu mkutano mkubwa wa hadhara wa kesho katika Viwanja vya
Jangwani, jijini Dar Es Salaam ambao umeshatangazwa kwa njia mbalimbali
za upashanaji habari, umeahirishwa hadi hapo maelekezo na utaratibu
mwingine utakapotolewa baadae.
Ni vyema kuwataarifu ujumbe huu mapema maelfu ya Watanzania ambao
tunajua wamejiandaa kuhudhuria kwa wingi kusikia 'neno kutoka kwa Rais
wa Mioyo ya Watanzania' na viongozi wakuu wa vyama vinavyounda UKAWA juu
ya uelekeo wa nchi kwenye mkutano huo ambao pia ulilenga kuwatambulisha
wabunge wote wa UKAWA na kuwashukuru Watanzania kwa namna walivyounga
mkono agenda za MABADILIKO kwenye mapambano makubwa ya ushindi wakiwa
begabega na Jemadari Lowassa, Babu Duni, wagombea ubunge na udiwani wa
UKAWA.
Hakuna maoni :