SIASA

SIASA

MAONI

MAONI

BURUDANI

MICHEZO

/ / UEFA CHAMPIONZ LIGI-LEO NANI KUPITA, ARSENAL VIPI, CHELSEA NINI?

>>PATA TATHMINI KUNDI KWA KUNDI!
UCL-SIT-SAFITAYARI Nafasi 3 kati ya 16 za Raundi ya Mtoano ya UEFA CHAMPIONZ LIGI, UCL, zimeshachukuliwa na Klabu 3 na bado zipo Klabu 27 kati ya 29 zilizobaki kwenye Makundi zenye nafasi za kuchukua Nafasi 13 zilizobaki.

 
KLABU ZILIZOFUZU KUINGIA MTOANO:
-Real Madrid
-Manchester City
-Zenit Saint Petersburg

IFUATAYO NI HALI YA KILA KUNDI KWA MECHI ZA JUMANNE NA JUMATANO:
Jumanne Novemba 24
KUNDI E:
-Barcelona (Pointi 10) v Roma (5)
-BATE Borisov (3) v Bayer Leverkusen (4)

Barcelona watasonga kama Washindi wa Kundi wakipata Sare na pia wanaweza kufuzu wakifungwa ikiwa Leverkusen watashindwa kushinda.

Ikiwa BATE na Leverkusen zitatoka Sare basi watupwa nje ya Timu mbili za juu ikiwa AS Roma watashinda.
Ikiwa BATE watafungwa na AS Roma kushinda, BATE watamaliza Nafasi ya 4.

KUNDI F:
-Bayern München (Pointi 9) v Olympiacos (9)
-Arsenal (3) v Dinamo Zagreb (3)
Sare kwa Bayern na Olympiacos itawatosha kutinga Raundi ya Mtoano.
Arsenal wanahitaji kushinda na kuombea Olympiacos wafungwe ili wapate nafasi ya kuifunga Olympiacos katika Mechi ya mwisho ya Kundi na wao kufuzu lakini inabidi ushindi uwe bora kuliko Olympiacos walipoifunga Arsenal 3-2 katika Mechi yao ya kwanza.
Arsenal hawawezi kuipita Bayern.

KUNDI G:
-Porto (Pointi 10) v Dynamo Kyiv (5)
-Maccabi Tel-Aviv (0) v Chelsea (7)
Porto watafuzu kwa Sare.
Chelsea watafuzu wakishinda na Dynamo kushindwa kupata ushindi.

KUNDI H:
-Zenit (Pointi 12, Washafuzu) v Valencia (6)
-Lyon (1) v Gent (4)
Zenit wameshafuzu na watatwaa Nafasi ya Kwanza ya Kundi wakishinda.
Valencia watafuzu wakishinda huku Gent wasishinde.

Jumatano Novemba 25
KUNDI A:
-Malmö (Pointi 3) v Paris Saint-Germain (7)
-Shakhtar Donetsk (3) v Real Madrid (10, Washafuzu)
Real Madrid wameshafuzu na watashinda Kundi hili wakiwa Namba 1 ikiwa watashinda au wakitoka Sare ikiwa PSG haishindi n ahata wakifungwa wanaweza kuwa Namba 1 ikiwa PSG itafungwa.
PSG watafuzu wakishinda au kwa Sare ikiwa Shakhtar haishindi.

KUNDI B:
-CSKA Moskva (Pointi 4) v Wolfsburg (6)
-Manchester United (7) v PSV Eindhoven (6)
Man United watafuzu wakishinda.
CSKA hawatafuzu wakifungwa. 

KUNDI C:
-Astana (Pointi 3) v Benfica (9)
-Atlético Madrid (8) v Galatasaray (4)
Benfica watasonga wakishinda na pia wakitoka Sare ikiwa Atletico itaifunga Galatasaray au kwenda Sare.
Ikiwa Benfica watashinda na Atletico hawashindi, basi Benfica watatwaa Nafasi ya Kwanza.
Atlético wanahitaji Sare kufuzu.

KUNDI D:
-Juventus (Pointi 8) v Manchester City (9, Washafuzu)
-Borussia Mönchengladbach (2) v Sevilla (3)
Man City wameshafuzu na watatwaa Nafasi ya Kwanza kwa ushindi.
Juventus watafuzu wakishinda au wakipata matokeo yeyote yale ili mradi Sevilla wasishinde.

Ili kuweka hai matumaini ya kufuzu, Sevilla lazima waifunge Mönchengladbach na kungojea Mechi ya mwisho na Juventus hapo Desemba 8 washinde ili wafuzu ingawa kwenye Mechi hiyo wasipoifunga Juve basi wabahakika ya kwenda EUROPA LIGI ambako walitwaa Ubingwa wake kwa Misimu Miwili iliyopita.
UCL-TEBO-NOV23
UEFA CHAMPIONZ LIGI
RATIBA
**Mechi zote kuanza Saa 4 Dak 45 Usiku, isipokuwa inapotajwa
Jumanne Novemba 24
KUNDI E
2000 BATE Borislov v Bayer Leverkusen          
Barcelona v AS Roma                 
KUNDI F
Arsenal v Dinamo Zagreb           
Bayern Munich v Olympiakos                
KUNDI G
FC Porto v Dynamo Kiev             
Maccabi Tel Aviv v Chelsea         
KUNDI H
2000 Zenit Saint Petersburg v Valencia           
Lyon v KAA Gent             
Jumatano Novemba 25
KUNDI A
Malmö FF v Paris St Germaine              
Shakhtar Donetsk v Real Madrid           
KUNDI B
2000 CSKA v VfL Wolfsburg        
Man United v PSV Eindhoven               
KUNDI C
1800 FC Astana v Benfica           
Atletico Madrid v Galatasaray               
KUNDI D
Borussia Mönchengladbach v Sevilla                
Juventus v Man City   

«
Next

Chapisho Jipya

»
Previous

Taarifa za zamani

About Unknown

Asante kwa kutembelea SELASINI HABARI,NITAKUHABARISHA, KUKUELIMISHA NA KUKUBURUDISHA HIVYO USIKOSE KUTEMBELEA SELASINIHABARI.BLOGSPOT.COM.

Hakuna maoni :

Leave a Reply