SIASA

SIASA

MAONI

MAONI

BURUDANI

MICHEZO

/ / UNAJUA KAMA STRAIKA MPYA SIMBA ANATUA NDANI YA SIKU CHACHE? SOMA HAPA


Uongozi wa Klabu ya Simba umeeleza kuwa unatarajia kumleta mshambuliaji mpya kutoka katika timu za hapa Bongo kwa ajili ya kufanya majaribio na iwapo atafuzu kocha Dylan Kerr atakuwa na jukumu la kumsajili.


Simba kwa sasa ipo katika mkakati mzito wa kufanya marekebisho katika kikosi chake kufuatia upungufu uliyojitokeza katika nafasi ya ushambuliaji kwenye michezo kadhaa ya ligi waliyocheza.

Mratibu wa Simba, Abass Ally, amesema wanatarajia kumpokea mshambuliaji huyo ndani ya wiki hii ili aanze majaribio.

“Kuna mchezaji anatarajia kutua ndani ya wiki hii kwa ajili ya kumfanyia majaribio ambaye anatoka katika timu za hapahapa Tanzania, anacheza nafasi ya ushambuliaji, hivyo kocha Kerr atakuwa na jukumu la kumuangalia uwezo wake na kufanya maamuzi.

“Mchakato uliopo Simba ni kuhakikisha tunafanikiwa kumaliza tatizo la ushambuliaji, hivyo iwapo mchezaji huyo ataonyesha uwezo basi tutamsajili,” alisema Abbasi.

Wakati huohuo, kiongozi huyo amesema wanampango wa kuwapeleka wachezaji watatu kwa mkopo ili waweze kusajili wengine.
 
“Kuna wachezaji watatu ambao wanatarajiwa kutolewa kwa mkopo, lakini wawili kati yao ndiyo wenye uwezekano mkubwa wa kuondoka kwa kuwa tayari tumeshawapatia timu.

“Lakini kuondoka kwao inategemea na makubaliano na wachezaji wenyewe iwapo watakubali kutolewa kwa mkopo kwani jambo hilo linahitaji maridhiano, lengo ni kuhakikisha tunafanikiwa kupata nafasi zaidi za kusajili,” alisema Abbas.

«
Next

Chapisho Jipya

»
Previous

Taarifa za zamani

About Unknown

Asante kwa kutembelea SELASINI HABARI,NITAKUHABARISHA, KUKUELIMISHA NA KUKUBURUDISHA HIVYO USIKOSE KUTEMBELEA SELASINIHABARI.BLOGSPOT.COM.

Hakuna maoni :

Leave a Reply