SIASA

SIASA

MAONI

MAONI

BURUDANI

MICHEZO

/ / UNAJUA KWA NINI KESSY ANASITA KUSAINI MKATABA MPYA SIMBA? MWENYE HUYU HAPA ANAFUNGUKA


Beki wa pembeni wa Simba, Hassani Kessy, amefunguka na kutaja sababu inayomzuia asiongeze mkataba ni timu hiyo kutoshiriki michuano ya kimataifa Afrika.


Kufikia mwezi ujao, Kessy atakuwa amebakiza miezi sita katika mkataba wake na kwa mujibu wa kanuni za Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa), anaruhusiwa kufanya mazungumzo na klabu nyingine inayomhitaji ikiwemo Yanga ambayo inatajwa kumuwania kwa ukaribu.

Yanga itashiriki katika Ligi ya Mabingwa Afrika kutokana na kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara msimu uliopita.

Kessy amesema mipango aliyojiwekea ni kucheza soka la kimataifa nje ya Tanzania na ndiyo maana amekuwa akisita kusaini mkataba mpya Simba.

“Sifikirii kuongeza mkataba wa kubaki kuendelea kuichezea Simba katika kipindi kingine, licha ya viongozi kuhitaji huduma yangu.

“Ninaamini kama nikipata timu inayoshiriki michuano ya kimataifa, basi bila kuchelewa nitasaini mkataba ili iwe rahisi kwaku kutimiza ndoto zangu kwa kuwa nitaonekana kimataifa,” alisema Kessy.

«
Next

Chapisho Jipya

»
Previous

Taarifa za zamani

About Unknown

Asante kwa kutembelea SELASINI HABARI,NITAKUHABARISHA, KUKUELIMISHA NA KUKUBURUDISHA HIVYO USIKOSE KUTEMBELEA SELASINIHABARI.BLOGSPOT.COM.

Hakuna maoni :

Leave a Reply