Aliyekuwa Katibu na Msemaji wa Chama cha Madereva, Rashid Saleh
amefariki dunia ghafla huku chanzo cha kifo chake kikizua utata miongoni
mwa wananchama wa chama hicho na wananchi.
Taarifa za awali kifo cha Rashid Swaleh zilielza kuwa alifariki baada ya kuugua ghafla ugonjwa ambao bado haujabainika.
Madereva na wananchi wengine walifika katika hospitali ya Muhimbili
wakiwa na majonzi makubwa huku wakisubiri mwili huo wa marehemu upimwe
ili kubaini chanzo cha kifo chake.
Baadhi ya madereva waliozungumza na waandishi wa habari walieleza
kusikitishwa na msiba huo wa ghafla na kueleza kuwa huenda msemaji wao
aliyekuwa anapigania kwa nguvu zote haki zao amenyamazishwa.
“Sisi kama madereva hatutakubali, kama kosa lake yeye ni kutetea haki za
watu, hili ni tatizo,” alisema mmoja wa madereva hao aliyejitambulisha
kwa jina la Shaban Mdem.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadick alifika katika hospitali
ya Taifa ya Muhimbili na kuwataka madereva hao kutokata tama bali
waendelee kudai haki zao huku wakisubiri majibu ya madaktari kubaini
chanzo cha kifo cha msemaji wao.
“Hii isiwakatishe tamaa kuendelea kudai haki zenu ambazo ni za msingi
kutoka kwa ajili wenu,” alisema huku akiwasihi kutofifishwa moyo katika
kutafuta haki zao za msingi.
Tagged with: MATUKIO
Hakuna maoni :