SIASA

SIASA

MAONI

MAONI

BURUDANI

MICHEZO

/ / WAARABU WAKANYAGANA ALGERIA WAKITANA KUMUONA MBWANA SAMATTA


Mashabiki wa soka jijini Algeria wamekanyagana wakitaka kumuona mshambuliaji hatari wa Taifa Stars, Mbwana Samatta.


Mashabiki hao kila mmoja alikuwa akitaka kumuona Samatta mara baada ya Taifa Stars kutua kwenye Uwanja wa Ndege wa Houari Boumediene jijini Algers.

“Yuko wapi Samatta, ni yule pale?” aliuza shabiki mmoja na kufanya wengi wakimbilie upande huo.

Samatta aliifunga USM Alger mara mbili katika mechi za fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika na kuiwezesha TP Mazembe kubeba ubingwa.

Tayari Stars imetua katika mji wa Bilda na kufikia katika hoteli ya nyota nne ya Hotel Ville Des Roses.


Stars itashuka dimbani keshokutwa kuwavaa Waarabu wa Algeria kuwania kucheza Kombe la Dunia ikiwa ni baada ya sare ya mabao 2-2 jijini Dar es Salaam.

«
Next

Chapisho Jipya

»
Previous

Taarifa za zamani

About Unknown

Asante kwa kutembelea SELASINI HABARI,NITAKUHABARISHA, KUKUELIMISHA NA KUKUBURUDISHA HIVYO USIKOSE KUTEMBELEA SELASINIHABARI.BLOGSPOT.COM.

Hakuna maoni :

Leave a Reply