SIASA

SIASA

MAONI

MAONI

BURUDANI

MICHEZO

/ / TAMBWE, KAVUMBAGU WAINGIA LAKINI WASHINDWA KUISAIDIA BURUNDI KUING'OA DR CONGO

KAVUMBAGU ANAYEKIPIGA AZAM FC, LEO AMEICHEZEA BURUNDI IKILALA DHIDI YA DR CONGO

Pamoja na Amissi Tambwe na Didier Kavumbagu kuingia katika kipindi cha pili wakati Burundi ikiivaa DR Congo, wameshindwa kuikomboa.

Burundi imefanikiwa kupata sare ya mabao 2-2 ikiwa ugenini katika mechi ya kuwania kucheza Kombe la Dunia nchini Russia.

Kavumbagu aliingia kuchukua nafasi ya Selemani Ndikumana aliyewahi kuichezea Simba huku Tambwe akiingikia kuchukua nafasi ya Gael Bigirimana.

Katika mechi ya kwanza, Burundi ililala kwa mabao 3-2 ikiwa nyumbani Bujumbura. Hivyo sare hiyo maana yake imeng’olewa kwa jumla ya mabao 6-5.

Katika mechi ya kwanza, Tambwe anayekipiga Yanga na Kavumbagu kutoka Azam FC, walimaliza dakika 90 wakiwa benchi.


Baada ya mechi hiyo, wachezaji hao wanalazimika kurejea nchini mapema na kuelekeza nguvu zao katika Ligi Kuu Bara.A

«
Next

Chapisho Jipya

»
Previous

Taarifa za zamani

About Unknown

Asante kwa kutembelea SELASINI HABARI,NITAKUHABARISHA, KUKUELIMISHA NA KUKUBURUDISHA HIVYO USIKOSE KUTEMBELEA SELASINIHABARI.BLOGSPOT.COM.

Hakuna maoni :

Leave a Reply