Fumbo kuhusiana na mtu mwenye sifa za kuwa Waziri Mkuu wa serikali ya
awamu ya tano ya Rais Dk. John Magufuli limeanza kufumbuliwa.
Hali hiyo inatokana na kile alichokidhihirisha Magufuli siku moja baada
ya kuapishwa kwake na pia baada ya hapo wakati alipochukua maamuzi
kadhaa ya vitendo, ikiwamo kutoa maelekezo muhimu yaliyodhihirisha aina
ya Waziri Mkuu atakayemteua.Kwa mujibu wa muundo wa serikali, Waziri
Mkuu ndiye kiongozi wa shughuli za serikali bungeni, ambaye mbali ya
kuwa kinara wa mawaziri wengine, ndiye anayetakiwa pia kutoa maamuzi
mazito linapojitokeza jambo linalomlazimu kufanya hivyo.
Wakizungumza na Nipashe, baadhi ya wafuatiliaji wa masuala ya siasa na
uongozi nchini wamesema hatua alizochukua Magufuli kuanzia siku ya
kwanza ya kuapishwa kwake zinatoa picha ya wazi aina ya watu atakaotaka
kuwa nao katika serikali yake.
Baada ya kuapishwa Novemba 5, 2015, kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es
Salaam, Dk. Magufuli alianza kazi siku hiyo hiyo kwa kutoa hotuba
iliyosisitiza juu ya kauli mbiu yake ya ‘hapa kazi tu’ katika kutumikia
wananchi, kuwafariji waliokuwa wapinzani wake katika urais huku
akiwasihi waungane naye kuijenga Tanzania imara na pia alimteua
Mwanasheria Mkuu, George Masaju, huku pia akitangaza siku ya kuanza
Bunge kuwa ni Novemba 17.
“Ratiba yake katika siku ya kwanza aliyoapishwa ilikuwa ngumu kutokana
na wageni wengi waliomtembelea lakini bado hakutaka kuchelewa katika
kuteua Mwanasheria Mkuu. Na siku iliyofuata (Ijumaa) akaonyesha yeye ni
Rais wa aina gani kwa kufanya ziara ya ghafla kwenye Wizara ya Fedha na
kujionea aina ya watendaji waliopo. Yote haya yanatosha
Tagged with: SIASA
Hakuna maoni :