SIASA

SIASA

MAONI

MAONI

BURUDANI

MICHEZO

/ / ADEBAYOR ALIPWA £100,000 KILA WIKI BILA KUICHEZEA SPURS!

ADEBAYOR2Emmanuel Adebayor bado analipwa Pauni Laki 1 kwa Wiki, takriban Shilingi 323, 853,238/=, na Tottenham licha ya kutoichezea tangu Machi 15.

Ikiwa hatajiunga na Klabu yeyote Mwezi Januari wakati Dirisha la Uhamisho litakapofunguliwa, Adebayor ataendelea kulipwa na Spurs Fedha ambazo zitafikia Jumla ya Pauni Milioni 5.25 ifikapo Juni Mwakani wakati Mkataba wake na Spurs utakapokwisha.

Straika huyo alitemwa na Tottenham Mwezi Septemba baada ya Meneja Mauricio Pochettino kutomsajili katika Vikosi vya Timu kwa ajili ya Ligi Kuu England na UEFA Europa Ligi.

Uamuzi huo ulimfanya Adebayor akatae kufanya Mazoezi na Kikosi cha Kwanza cha Spurs na kumshangaza kila Mtu kuamua kufanya Mazoezi na Timu za Vijana za Spurs.

Emmanuel Adebayor-Ndani ya Soka:
Umri: 31
Uraia: Togo
Klabu:
Metz (2001-2003): Mechi 53, Magoli 19
Monaco (2003-2006): Mechi 115, Magoli 26
Arsenal (2006-2009): Mechi 142, Magoli 62
Man City (2009-2012): Mechi 45, Magoli 19
Real Madrid (2011): Mechi 22, Magoli 8
Tottenham (2011-15): Mechi 106, Magoli 41

Septemba Mosi, Siku ya mwisho ya Dirisha la Uhamisho, Adebayor, alikuwa na nafasi ya kujiunga na West Ham lakini aligoma kuondoka akitaka kwanza alipwe Pauni Milioni 5.

Tangu atemwe na Spurs, Adebayor amekuwa akitumia muda wake akiwa kwao Togo na Ghana huku mara kwa mara akiposti Picha kwenye Mitandao akila raha na wakati mwingine kucheza Soka.

«
Next

Chapisho Jipya

»
Previous

Taarifa za zamani

About Unknown

Asante kwa kutembelea SELASINI HABARI,NITAKUHABARISHA, KUKUELIMISHA NA KUKUBURUDISHA HIVYO USIKOSE KUTEMBELEA SELASINIHABARI.BLOGSPOT.COM.

Hakuna maoni :

Leave a Reply