MZEE DALALI AKIWA KWENYE UWANJA WA NANGWANDA MJINI MTWARA, LEO. |
Mwenyekiti
wa zamani wa Simba, Hassan Dalali, amelaani kwa kiasi kikubwa vurugu
walizofanyiwa wachezaji na makocha wa Simba mjini Mtwara.
Dalali
maarufu kama Fiel Marshal amezungumza na SALEHJEMBE kutoka mjini Mtwara
na kusema kwake ameona ni maajabu ya karne kwa vurugu na dharau kubwa
walizofanya mashabiki hao wa Ndanda.
Taarifa
nyingine zimesema Jeshi la Polisi mkoani Mtwara, limewakamata na
kuwatia mbaroni watu watatu ikiwa ni kati ya wale waliokuwa wakiwafanyia
Simba vurugu.
“Niko
hapa Mtwara, kwa kweli hali ilikuwa mbaya sana, hawa watu hawakuwa
wastaarabu hata kidogo. Wamefanya mambo ya ajabu mimi sijaona katika
kipindi changu chote cha uongozi wa soka.
“Wameingia uwanjani na kuwatukana sana wachezaji, wametukana matusi ya nguoni lakini niwapongeze wachezaji walivumilia sana.
“Walishuka hadi kwenye benchi la Simba pale, wakatukana sana, wakahamia jukwaani nako wakatukana sana.
“Hiyo
haikutosha, wakati tunatoka wakaanza kutushambulia kwa mawe, sasa
uzalendo ukawashinda vijana. Wakashuka na kuwakimbiza, wakawashika
watatu na kuwazuia hadi Polisi walipofika pale, wakawaweka kizuizini.
“Kabla
ya hapo, wachezaji walilazimika kusubiri saa zima ili kuingia kwenye
uwanja kwa ajili ya mazoezi. Uongozi wa uwanja ulikuwa unazungusha na
wale mashabiki walikuwa pale wakisema wazi kwamba hatutafanya mazoezi
hapo kwa kuwa wameweka mambo yao ambayo sijui ni yapi,” alisema Dalali.
“Kweli
hali haikuwa nzuri, mambo yalikuwa mabaya sana na washukuru mashabiki
wa Simba kutoka Dar es Salaam hawakuwa wamefika. Ingekuwa maafa kwa
kweli, tumshukuru sana Mungu.
“Lakini
vipi watu wafanye Simba kama iko nchi jirani, nafikiri wanapaswa
kuadhibiwa na kama ni sheria hakika ichukue mkondo wake,” alisema Dalali
akionyesha kuchukizwa na jambo hilo.
Kali
hali isiyokuwa ya kawaida, wachezaji wa Simba walijikuta katika wakati
mgumu baada ya kuvamiwa na mashabiki wa Ndanda wakati wakifanya mazoezi
kwenye Uwanja wa Nangwana Sijaona mjini Mtwara, jioni hii.
Hakuna maoni :