Kali
hali isiyokuwa ya kawaida, wachezaji wa Simba wamejikuta katika wakati
mgumu baada ya kuvamiwa na mashabiki wa Ndanda wakati wakifanya mazoezi
kwenye Uwanja wa Nangwana Sijaona mjini Mtwara, jioni hii.
Kabla
ya hapo, wachezaji wa Simba walilazimika kusubiri kwa zaidi ya saa moja
baada ya uongozi wa Uwanja wa Nangwana kugoma kuwafungulia mlango.
“Baada ya juhudi za ziada, mlango ulifunguliwa kwa kuwa ni sheria kwamba tunaruhusiwa kuutumia siku moja kabla ya mechi.
“Ajabu
tulizuiwa, baada ya juhudi binafsi ukafunguliwa na wakati tunaanza
mashabiki hao nao waliingia na kuanza kuporomosha matusi makali sana.
“Wachezaji
walikuwa wavumilivu wakaendelea na mazoezi, wale watu wakahama pale na
kwenda jukwaani. Kule walikaa nako wakaendelea kutukana sana, bado kila
mtu alikuwa mvumilivu,” alieleza mmoja wa watu walioongoza na kikosi cha
Simba mjini Mtwara.
“Baada
ya kumaliza mazoezi wakati tunatoka, ndipo wakaanza kurusha mawe katika
basi na magari mengine. Baadhi ya watu wakashuka na kuanza
kuwakimbiza.”
“Kwa kweli tumefanyiwa vurugu sana, unyanyasaji wa wazi na hiki ni kitu cha ajabu kabisa.”
Simba inatarajia kushuka dimbani kesho kuivaa Ndanda pia ni haki yao kuutumia uwanja huo kwa mazoezi yao leo.
Hakuna maoni :