SIASA

SIASA

MAONI

MAONI

BURUDANI

MICHEZO

/ / Je, Huu Sio Uvunjaji wa Haki Za Msingi za Binaadamu Unaofanywa na Serikali ya Magufuli?

Kama jambo hili ni kweli limefanyika: Kigogo wa BoT azuiwa Airport kutokana na kukosa vibali vya kusafiri nje ya nchi


Haiwezekani mtu ambaye yuko huru, tena yuko likizo, ameamua kwenda kujipumzikia zake nchi za wenzetu, azuiliwe!.

Nafahamu kuna wafanyakazi wa serikali, na baadhi ya idara nyeti, au hata madakitari, jeshi, polisi na zimamoto, hata wakiwa likizo, wanawajibika kumtaarifu mwajiri wao, likizo yake atakuwa wapi, ili in case of anything, aweze kuwa reached out!, lakini kitendo cha maofisa uhamiaji, kumzuia mtu mwingine yoyote wa serikali, asisafiri nje ya nchi, huu ni ukiukwaji wa haki za msingi za binaadamu!.

Pamoja na nia nzuri, na nia njema ya Rais wetu, Dr. John Pombe Magufuli, kudhibiti safari za nje ya nchi zisizo na tija kwa taifa, utekelezaji wa kauli hiyo, lazima uzingatie taratibu, sheria na kanuni, na sio kutekelezwa tuu kama zimamoto, na kukiuka haki za msingi za binadamu!.

Ila pia niliwahi kushauri humu, kama baadhi ya sheria, zinaweza kuwa ni kikwazo kwa rais wetu, kututengeneza Tanzania tunayoitaka, rais anayo mamlaka ya kisheria, kuandika waraka, 'decree' kuiweka kando katiba , hivyo kuitawala Tanzania kwa kutumia decree hivyo kuwa huru kufanya jambo lolote atakavyoona inafaa!.
Mhe. Rais futilia mbali utawala wa sheria Ongoza Kwa Kutumia Decree tuu!


Viongozi wote wanakula kiapo cha utii wa katiba!, kama katiba inatoa uhuru fulani!, haiwezekana, akaibuka mtu mwingine, kwa mamlaka aliyopewa na katiba hiyo, akauondoa uhuru fulani na haku tunamtazama tuu, au tunamshangilia!. Hili haliwezekani!.

Japo wengi wetu, tunaishi katika lindi la umasikini, uliotopea, na sio tuu hatuna hata hiyo likizo, lakini umasikini wetu, usutufanye tuwachukie, wenzetu waliobahatika kuwa wenye heri, wenye uwezo wa kwenda kujipumzikia zao ulaya wakati wa likizo zao!.

Nashauri serikali itoe waraka wa ufafanuzi wa hili katazo la safari za nje, unless itamkwe wazi, watumizi wote wa umma, hata safari zao binafsi kujipumzikia, au kuwatembelea wapendwa wao, wapenzi wao au hata vimada wao, sasa lazima waombe kibali kwa KMK!, na jee kama hivi ndivyo katiba ilivyotamka?!, kama sio kwa mujibu wa katiba, then rais atoe waraka, Tanzania tujijue tuko kama China au Urusi, enzi zile, kuingia Beijing au Moscow, mtu hujiingilii hivi hivi!.

Jee kumkumbusha rais wetu kuhakikisha watendaji wake wanazingatia katiba aliyoapa kuilinda, ni kumuingilia katika utendaji wake?!.

Pasco/Jamii Forums

«
Next

Chapisho Jipya

»
Previous

Taarifa za zamani

About Unknown

Asante kwa kutembelea SELASINI HABARI,NITAKUHABARISHA, KUKUELIMISHA NA KUKUBURUDISHA HIVYO USIKOSE KUTEMBELEA SELASINIHABARI.BLOGSPOT.COM.
1 maoni
  1. Du!, hii kitu ni ya siku nyingi na ni yangu mwenyewe, leo ndio nimekutana nayo huku!.

    JibuFuta