Kocha Mkuu wa Kilimanjaro
Stars, Abdallah Kibadeni amesema Ethiopia haikuwa na uwezo wa kukifunga kikosi
chake, lakini walibebwa na Cecafa.
Kibadeni amesema Cecafa
ilionyesha wazi ilitaka kuona Ethiopia wanafika mbali licha ya kuwa na kikosi
kibovu.
Pamoja na hivyo, Kibadeni
amesema hakuwampanga mshambuliaji Elius Maguri katika mechi ya pili ya Ethiopia
hatua ya robo fainali kwa kuwa alikuwa na kadi mbili.
“Maguri na Aishi Manula
walikuwa na kadi mbili za njano, lakini Barthez (Ally Mustapha) alikuwa
mgonjwa,” alisema Kiabadeni.
Stars ilimaliza mechi zote mbili dhidi ya Ethiopia kwa sare ya 1-1 lakini hatua ya robo fainali ikatolewa kwa mikwaju ya penalti 4-3.
Hakuna maoni :