VAN GAAL AKIINUKA NA KUONDOKA KATIKA MKUTANO WA WAANDISHI WA HABARI BAADA YA KUUENDESHA KWA DAKIKA 4 NA SEKUNDE 58 TU. |
Louis van Gaal sass mambo yanaonekana kumshinda England.
Maana amejikuta akiinuka na kuondoka wakati wa mkutano wa waandishi wa habari uliofanyika katika klabu ya Manchester United.
Van
Gaal alilazimika kufanya hivyo baada ya kuulizwa anazungumziaje suala la
kutemwa iwapo atafungwa na Stoke City na nafasi take ichukuliwe na Jose
Mourinho.
Wakati
mkutano huo wa waandishi ulikuwa umefanyika kea dakika 4 na sekunde 58,
van Gaal aliinuka na kuondoka, huku akisema “tutaonana mwakani.”
Akikiongoza
kikosi cha Man United, kimepoteza mechi tatu mfululizo na kukifanya
kionekane kuwa taabani naye si mkombozi kama ilivyozoeleka.
Sasa
Kocha Mourinho ambaye yuko huru baada ya kutemwa na Chelsea ndiye
anapewa nafasi kubwa ingawa makocha wengine kama Pep Guardiola
wanatupiwa macho na Manchester United.
Hakuna maoni :