SIASA

SIASA

MAONI

MAONI

BURUDANI

MICHEZO

/ / MAMBO YAMSHINDA VAN GAAL, MASWALI YA WAANDISHI YAMKIMBIZA KWENYE MKUTANO, AONDOKA NA KUWAACHA SOLEMBA


VAN GAAL AKIINUKA NA KUONDOKA KATIKA MKUTANO WA WAANDISHI WA HABARI BAADA YA KUUENDESHA KWA DAKIKA 4 NA SEKUNDE 58 TU.

Louis van Gaal sass mambo yanaonekana kumshinda England.

Maana amejikuta akiinuka na kuondoka wakati wa mkutano wa waandishi wa habari uliofanyika katika klabu ya Manchester United.

Van Gaal alilazimika kufanya hivyo baada ya kuulizwa anazungumziaje suala la kutemwa iwapo atafungwa na Stoke City na nafasi take ichukuliwe na Jose Mourinho.

Wakati mkutano huo wa waandishi ulikuwa umefanyika kea dakika 4 na sekunde 58, van Gaal aliinuka na kuondoka, huku akisema “tutaonana mwakani.”

Akikiongoza kikosi cha Man United, kimepoteza mechi tatu mfululizo na kukifanya kionekane kuwa taabani naye si mkombozi kama ilivyozoeleka.

Sasa Kocha Mourinho ambaye yuko huru baada ya kutemwa na Chelsea ndiye anapewa nafasi kubwa ingawa makocha wengine kama Pep Guardiola wanatupiwa macho na Manchester United.

«
Next

Chapisho Jipya

»
Previous

Taarifa za zamani

About Unknown

Asante kwa kutembelea SELASINI HABARI,NITAKUHABARISHA, KUKUELIMISHA NA KUKUBURUDISHA HIVYO USIKOSE KUTEMBELEA SELASINIHABARI.BLOGSPOT.COM.

Hakuna maoni :

Leave a Reply