Watanzania
wanaokipiga klabu ya TP Mazembe ya nchini Congo DR wameshuhudia timu
yao ikishindwa kupata ushindi kwa mara nyingine kwenye michuano ya FIFA
Club Word Cup kufuatia kukubali kichapo kingine cha pili cha magoli 2-1
kutoka kwa Club America ya Mexico.
Samatta
na Ulimwengu wote walianza kikosi cha kwanza cha TP Mazembe dhidi Club
America, lakini wao na wenzao hawakuweza kufua dafu mbele ya wanaume hao
wa Mexico.
Magoli
ya Dario Benedetto pamoja na Martin Zuniga yameipa America ushindi wa
bao 2-1 dhidi ya TP Mazembe na kufanikiwa kuwa mshindi wa tano wa kwenye
mashindano hayo mwaka 2015.
Mabingwa
hao wa CONCACAF walichezea kichapo cha dakika za lala salama kutoka kwa
Guangzhou Evergrande Taobao kwenye mchezo wao wa robo fainali lakini
shukrani zinaenda kwa Dario Benedetto na Martin Zuniga kwa kuisaidia
timu yao kuibuka na ushindi.
Benedetto
aliipa America bao la kuongoza dakika ya 20 kipindi cha kwanza na
wakaongeza bao la pili kupitia Zuniga ambaye aliingia kipindi cha pili.
Rainford
Kalaba aliifungia Mazembe bao la kufutia machozi kabla ya mapumziko
lakini Club Amerika walionekana kutawala sehemu kubwa ya mchezo huo.
Matokeo
hayo yanaiacha TP Mazembe ikiwa nafasi ya sita ikiambulia dola za
kimarekani milioni moja wakati Club Amerika yenyewe imefanikiwa kumaliza
mashindano hayo ikiwa nafasi ya tano na kujinyakulia dola la kimarekani
milioni moja na nusu.
Timu
ya Auckland City baada ya kufungwa na Sanfrecce Hiroshima kwenye mchezo
wa kwanza wenyewe moja kwa moja wanashika nafasi ya saba na kutokana na
kushika nafasi hiyo wanajinyakulia kitita cha dola laki tano za
kimarekani.
Hakuna maoni :